Mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden amezungumza na umma wa Wamarekani na kutahja tena vipaumbele vyake katika kipindi hiki akiashiria ushindi wa urais.
Pamoja na kusema zoezi la kuhesabu kura halijakamilika lakini mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Bide amesema hatua ya ushindi inayoashiria ndio inafungua njia ya zingatio la kubaliana na janga la corona, ubaguzi na mabadiliko ya tabia nchi miongoni mwa mambo mengine. Mgombea huyo ameyasema hayo wakati kumekuwa na ishara ya ushindi katika majimbo muhimu, wakati kwa upande wa mpinzani wake akiendelea kulalamikia kuchezewa rafu, na kutaka majimbo hayo kusimamisha zoezi la kuhesabu kura. Mpaka wakati huu Biden anahitaji kura sita za wajumbe wa majimbo ilikufikia 270 inayohitajika kumuingiza Ikulu.
Katika jimbo la Arizona ambako asilimia 94 za kura zimehesabiwa Biden ana asalimia 49.9 na Trump asilimia 48.6. Pennsylavania ambako wapo katika asilimia 96 Trump ana asilimia 49.2 na Biden 49.5. Georgia ambako kumehisabiwa kwa asilimia 99 Biden ana asilimia 49.5 na Trump, 49.4 North Carolina kushahesabiwa asilimia 98 na Trump kapata asilimia 50.0 Biden ikiwa 48.6, Nevada asilimia 93 Trump kapata 48.0 na Biden 49.8.
Tayari kwa upande wa Pennsylavania chama cha Republican kimeitaka Mahakama Kuu kuwasimamisha maafisa wa uchaguzi, kusimamisha kura ambazo ziliwasilisha katika maeneo ya kuhesabu kura baada ya kupita siku ya uchaguzi. Kiongozi mwenye dhamana na masuala ya nje wa jimbo hilo, kwamba maafisa wote wa vituo vya kuhesabu kura katika jimbo hilo wameamrishwa kutimiza takwa hilo, Ingwa kwa upande wa Republican wanasema hakujawa na uhakika wa jambo hilo kutelezwa na maafisa wote. Lakini kabla ya uchaguzi huo, mahakama ya kuu ya Pennyslavania iliidhinisha kwamba kura zilizopigwa siku ya uchaguzi na zikafika katika maeneo ya vituo hata kama zitawasili vituoni ndani ya siku tatu.
Katika matukio mawili tofauti, Mahakama Kuu ya Marekani imekataa kuingiliwa, kufuata maombi ya Republican ya kugeuza uamuzi. Timu ya kampeni ya Donald Trump ipo katika mchakato wa kushiriki makabiliano ya kisheria, lengo likiwa ni uhalali kuwasili baada ya uchaguzi kwa kura zilizopigwa katika jimbo la Pennyslavania. Takwa hilo la kisheria la Republican linahusu rundo la kura zilizopigwa kwa njia ya posta, kutoka upande wa Pennyslavania, ambalo linajumuisha mji wa pili kwa ukubwa wa Pittsburgh.
Watu wawili wenye kujihami na sialaha wametiwa mbaroni, karibu na eneo ambalo kunahesabiwa kura ambazo zinatahamua nani atakuwa rais wa taifa hilo kati ya Rais Donald Trump na Joe Biden. Kwa mujibu wa polisi waliotiwa mbaroni ni Joushua Macias mwenye umri wa miaka 42 na Antonia LaMotta mwenye umri wa miaka 51. Wote wanatajwa kutoka maeneo ya Virginia, na kwamba hawakuwa na kibali cha kubeba silaha hizo zilizokuwa zimesheheni risasi. Wote kwa pamoja wameswekwa rumande wakisubiri mashitaka yao.
Lakini pia duru zinamnasibisha ufuwasi wa Trump kwa kuwa mmoja kati ya watuhumiwa hao wawili, kabla ya kukamatwa alisambaza picha katika ukurasa wake wa Facebook akiwa nje ya jengo la kuhesabu kura katika mji huo wa Philadelphia, akiwa amevaa fulana yenye picha ya Trump.
Source