Wednesday, November 25, 2020

Picha : KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AFUNGUA KONGAMANO LA AFYA DODOMA....AGPAHI YASHIRIKI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto  Profesa Mabula Nchembe akifungua Kongamano la Afya nchini  (Tanzania Health Summitt) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Nchembe amefungua Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summitt) litakalojikita katika kujadili masuala mbalimbali ya afya hasa katika kipindi hiki ambacho nchi imeingia katika uchumi wa kati. 

Kongamano hilo litakalofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia leo Jumatano Novemba 25,2020 hadi Novemba 26,2020 linafanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma limekutanisha pamoja wadau wa sekta ya Afya kutoka taasisi za umma,Mashirika ya dini na binafsi. 

Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi ni Miongoni mwa wadau wa afya wanaoshiriki katika Kongamano hilo linaloongozwa na Kauli Mbiu ya "Mafanikio ya Uchumi wa Kati Katika Kuweka Afya Bora kwa Watanzania – Transforming The Success of Middle – Income Economy Into a Healthier Nation)"

Akizungumza wakati wa kufungua Kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Nchembe amesema licha ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa na serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi lakini bado kuna baadhi ya watu wanashindwa kuvifikia vituo vya afya na kupata huduma za afya. 

"Naomba mtumie kongamano hili kujadili ni namna gani tutoe huduma bora za afya,namna gani tuboreshe vifaa,miundo mbinu katika hospitali zetu.Namna gani tufanye ili kila mtu apate huduma za fya",amesema Prof. Nchembe. 

"Kupitia kongamano hili tujadili na kutoa mapendekezo ya namna ya kuwasaidia kupata huduma za afya watu wa hali ya chini wakiwemo wakulima ambao hawawezi kufikia huduma za afya na hawana na bima za afya",ameongeza Prof. Nchembe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto  Profesa Mabula Nchembe akifungua Kongamano la Afya nchini  (Tanzania Health Summitt) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto  Profesa Mabula Nchembe akifungua Kongamano la Afya nchini  (Tanzania Health Summitt) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto  Profesa Mabula Nchembe akifungua Kongamano la Afya nchini  (Tanzania Health Summitt) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto  Profesa Mabula Nchembe akifungua Kongamano la Afya nchini  (Tanzania Health Summitt) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi wakiwa kwenye Kongamano la Afya jijini Dodoma leo Novemba 25,2020.

Wadau wa afya wakiwa kwenye Kongamano la Afya jijini Dodoma leo Novemba 25,2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto  Profesa Mabula Nchembe akifungua Kongamano la Afya nchini  (Tanzania Health Summitt) leo Novemba 25,2020 katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Wadau wa afya wakiwa kwenye kongamano.
Wadau wa afya wakiwa kwenye kongamano la afya.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe akizungumza kwenye Kongamano la Afya nchini linalofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe akizungumza kwenye Kongamano la Afya nchini linalofanyika jijini Dodoma.
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kongamano la Afya.
Wadau wa afya wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii, Peter Maduki akizungumza kwenye Kongamano la Afya.
Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii, Peter Maduki akizungumza kwenye Kongamano la Afya.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kongamano la afya.
Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Nchembe akijiandaa kukabidhi vyeti kwa washiriki wa Kongamano la afya.
Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Nchembe akimkabidhi  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la AGPAHI, Alio Hussein ambaye ni Meneja Mradi AGPAHI mkoa wa Mara cheti cha Ushiriki wa Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summitt).

Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Nchembe akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe cheti cha Ushiriki wa Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summitt).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Nchembe akipiga picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Afya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Nchembe akipiga picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Afya.
Wafanyakazi wa AGPAHI wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe (wa tatu kulia).
Awali Meneja Mradi AGPAHI mkoa wa Mara (kushoto) , Alio Hussein akiwasili katika Kongamano la Afya.
Wafanyakazi wa AGPAHI wakiwa kwenye kongamano la afya.
Wafanyakazi wa AGPAHI wakiwa kwenye kongamano la afya.
Wadau wa afya wakiwa kwenye kongamano la afya.
Wadau wakiwa kwenye kongamano la afya

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...