Sunday, November 8, 2020
Kidato cha pili kuanza mtihani kesho
Jumla ya watahiniwa 646,148 wa kidato cha pili kesho Novemba 9, wanatarajiwa kuanza mtihani wa upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili huku kidato cha Nne wakianza mtihani wa taifa Novemba 23 hadi Desemba 11, mwaka huu.
Akitoa ratiba hiyo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza Mitihani la Tanzania (NECT), Dk. Charles Msonde amesema mtihani wa upimaji wa darasa la nne unatarajiwa kufanyika kwenye shule 4,948 za Sekondari Tanzania Bara na kwamba maandalizi yote yamekamilika.
Amesema kati ya watainiwa hao, wavulana ni 301,831 sawa na asilimia 46.71 huku wasichana wakiwa 344,317 sawa na asilimia 53.29.
"Mitahini hii inanza kesho Novemba 9 hadi 20 mwaka huu, aidha, wapo watainiwa wenye mahitaji maalum 731 na kati yao 406 ni wenye uoni hafifu, 55 ni wasiona, watatu ni wenye ulemavu wa kusikia na 267 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili.
"Mwaka 2019 idadi ya watainiwa waliosajiliwa walikuwa 609,502, hivyo kuna ongezeko la jumla ya watainiwa 36, 646 sawa na asilimia 5.7 kwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana," amesema Dk. Msonde.
Amesema mtihani wa taifa wa kidato cha Nne na Maarifa(QT) utafanyika Novemba 23 hadi Desemba 11, mwaka huu katuka jumla ya shule za sekondari na vituo vya mitihani 6,727 Tanzania Bara na Zanzibar.
"Jumla ya watainiwa 490,103 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha Nne mwaka huu ambapo kati yao watainiwa wa shule ni 448,164 na watainiwa wa kujitegemea ni 41,939.
"Kati yao watainiwa wa shule ni 448,164 waliosajili, wavulana ni 213, 553 sawa na asilimia 47.7 na wasichana ni 234,611 sawa na asilimia 52.3.
"Aidha, wapo watainiwa wenye mahitaji maalum 893 na kati yao 425 ni wenye uoni hafifu , 60 ni wasioona, 186 wenye ulemavu wa kusikia na 222 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili," alisema Dk. Msonde.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
