Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa Al-Kazimi, ametangaza kwamba serikali ya Marekani imeondoa wanajeshi 2500 waliokuwa nchini humo.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha Al-Iraqiyya, Kazimi alisema kuwa Iraq imefanikiwa kuingia maafikiano ya kimikakati na serikali ya Marekani kuhusu suala hilo.
Kazimi alisema, ''Vikosi vya jeshi la Marekani vimekubali kuacha kambi za kijeshi za Iraq na kuamua kuondoa wanajeshi 2500 waliokuwa nchini humo. ''
Rais wa Marekani Donald Trump, aliwahi kufanya mazungumzo na waandishi wa habari mnamo tarehe 20 Agosti kabla ya kukutana na Waziri Mkuu Kazimi White House, na kusema, ''Tunataka kuondoa wanajeshi wetu Iraq haraka iwezekanavyo. Tunasubiria kwa hamu siku hiyo itakapofika.''