Rais wa mpito nchini Mali, Bah Ndaw, ameteua serikali ya watu 25 ambapo maafisa waandamizi wa jeshi wamepewa nyadhifa muhimu.
Kulingana amri ya rais iliyosomwa kupitia kituo cha televisheni cha taifa, wizara za ulinzi, usalama, utawala wa maeneo na maridhiano ya kitaifa zote zikiwa zinaongozwa na makanali wa jeshi la Mali.
Bwana Ndaw – ambaye aliongoza jeshi la anga – alichaguliwa kuwa rais wa nchi na kiongozi wa mapinduzi.
Kufuatia kuchaguliwa kwa waziri mkuu ambaye ni raia, mamlaka za kikanda kama vile ECOWAS – inatarajiwa kuondolea nchi hiyo vikwazo ilivyoiwekea baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Agosti.
kanali Sadio Camara, mmoja wa viongozi wa waliopindua serikali, atakuwa waziri wa ulinzi, huku msemaji wa jeshi wa kundi hilo hilo, kanali Maj Ismaël Wagué, akipewa fursa ya kusimia maridhiano ya kitaifa.
Baadhi ya nyadhifa nyingine muhimu pia ziliwaendea aliyekuwa mwendesha mashtaka, Mohamed Sidda Dicko, akipewa nafasi ya idara ya sheria.
Na nyadhifa nne tu zilizopewa wanawake huku mbili tu zikitengwa kwa upinzani, M5, ambao uliongoza maandamano yaliyopelekea kumng'oa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta aliyepinduliwa na jeshi.