Thursday, October 8, 2020

Mshukiwa wa mauaji ya mtu mweusi nchini Marekani George Floyd aachiliwa kwa dhamana


Polisi wa zamani wa Marekani aliyeshitakiwa kwa mauaji ya mwanamume mweusi ambaye hakuwa amejihami George Floyd ameachiliwa kutoka jela kwa dhamana.

Derek Chauvin alitoa Bondi ya dola milioni moja sawa na (Euro 774,000) na kuachiliwa Jumatano asubuhi, nyaraka za mahakama zinaonesha.

Afisa huyo mzungu alirekodiwa kwenye kanda ya video akipiga goti kwenye Shingo ya Bw. Floyd kwa karibu dakika nane kabla afariki dunia Mei 25.

Kifo cha Bw. Floyd kilisababisha maandamano makubwa nchini Marekani kushinikiza mageuzi katika idara ya polisi, yakiongozwa vugu vugu la Black Lives Matter.

Bw Chauvin alifutwa kazi na sasa anasubiri hukumu dhidi yake baada ya kushitakiwa kwa mauaji ya kiwango cha pili na kuua bila kukusudia mwezi machi. Maafisa wengine watatu - J Alexander Kueng, Thomas Lane na Tou Thao - pia walifutwa kazi na kushitakiwa kwa kutowajibika tukio la mauaji likifanyika mbele yao.

Maafisa wote wanne wanaotuhumiwa kwa mauaji ya Bw. Floyd huko Minneapolis, Minnesota, wamelipa dhamana na wako huru wakisubiri hukumu dhidi yao kutolewa mwaka ujao.

Chauvin alikuwa anazuiliwa katika jela ya Oak Park Heights, Minnesota, tangu mwishoni maw mwezi Mei.

Mnamo mwezi Juni, jaji iliweka dhamana ya dola milioni 1.25 bila masharti, ama dola milioni moja ambayoo ilijumuisha masharti ya Bw Chauvin kutowasiliana na familia ya Bw. Floyd, kupeana silaha yake na kutofanya kazi katika idara ya sheria ama ya usalama akisubiri hukuku dhidi yeke.

Bw. Chauvin aliachiliwa kwa dhamana ya masharti, ambayo nyaraka za mahakama zinaonesha ilihakikiwa na wakala wa dhamana, Kituo cha habari cha CBC kiliripoti.

Nchini Marekani, wakala wa dhamana anaahidi kulipa mamlaka kiwango kamili cha dhamana kwa washitakiwa ikiwa hawana uwezo wa kufanya hivyo auwatashindwa kufika mahakamani.

Bw. Chauvin alittolewa kizuizini muda mfupi kabla ya saa tano na nusu asubihi (saa za Marekani) siku ya Jumatano,kwa mujibu wa ofisi ya polisi ya kaunti ya Hennepin.

Ben Crump, wakili na mwanaharakati wa kutetea haki anayewakilisha familia ya Bw. Floyd, alisema kuachiliwa kwa Chauvin kwa dhamana "inatukumbusha kwa machungu" kwamba "bado tuko mbali kupata haki kwa George".

"Japo George Floyd alinyimwa haki akiwa hai, hatututarudi nyuma hadi atendewe haki akiwa amekufa," Bw Crump alisema.

Kwa sasa, maafisa wote wanne wamepangiwa kuhukumiwa pamoja mwezi Machi, lakini jaji inatafakari uwezekano wa kila mmoja wao kuhukumiwa kivyake.

Tukio lililosababisha kushitakiwa kwao lilitonesha makovu ya ubaguzi na ukosefu wa usawa nchini Marekani.

Maandamano ya Black Lives Matter - ambayo baadhi yallikumbwa na vurugu - ilikuwa suala la kisiasa kuelekea uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba Marekani.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...