Wednesday, September 30, 2020
HESLB Yatoa Siku Tano (05) Kwa Wahitimu Mafunzo Jkt Kuomba Mikopo
Na Mwandishi Wetu, HESLB
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa muda wa siku 5 kuanzia Oktoba mosi hadi 5 mwaka huu ili kuwawezesha wanafunzi waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hivi karibuni kuingia katika mfumo wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao na kukamilisha maombi yao.
Katika taarifa yake aliyotoa kwa vyombo vya habari leo Jumatano (Septemba 30, 2020) Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru alisema uamuzi huo unatokana na maombi ya wanafunzi, wazazi na walezi ambao hawakuweza kuomba au kukamilisha maombi yao kutokana na sababu ya kujiunga na mafunzo hayo.
Kwa mujibu wa Badru alisema katika muda huo wa siku tano, mfumo pia utakuwa wazi ili kuwawezesha waombaji ambao maombi yao yana upungufu kurekebisha kwa kuweka nyaraka sahihi ili kuiwezesha HESLB kuendelea na hatua nyingine.
"Kwa wanaorekebisha taarifa, wanapaswa kuingia katika akaunti zao walizofungua kuombea mkopo na watapata ujumbe kuhusu maeneo ya kurekebisha. Tunawasihi watumie muda huu wa siku tano kurekebisha na kukamilisha maombi yao'' alisema Badru.
Katika mwaka wa masomo 2020/2021, Serikali imetenga TZS Bilioni 464 zitakazowanufaisha jumla ya wanafunzi 145,000. Kati yao, wanafunzi 54,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na wengine 91,000 ni wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo. Mwaka 2019/2020 jumla ya TZS 450 bilioni zilitengwa na zimewanufaisha jumla ya wanafunzi 132,119.
MWISHO
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...