Aliyekuwa Rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) Fatma Karume amemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi kutaja kifungu cha sheria kilichovunjwa na wanachama wa chama CHADEMA.
Fatma amesema hayo kupitia ujumbe wake alituma kwenye ukurasa wake twitter na kutaka kutoa ufafanuzi ili wanachama wa chama hicho kujua kosa lao.
"Francis ni mwanasheria angeanza kwa kutaja ibara ya Katiba iliyovunjwa na kipengele cha sheria kilichovunjwa ili wananchi waelewa" Ameandika Karume.
Mapema leo Agosti 4, 2020 msajili huyo wa vyama vya siasa alituma onyo kwa chama cha CHADEMA juu ya kitendo chao cha kuongeza beti kwenye wimbo wa Taifa.
Francis ni Mwanasheria angeanza kwa kutaja ibara ya Katiba iliyovunjwa na kipengele cha SHERIA kilichovunjwa ili WANANCHI waelewa. https://t.co/wpD39Jxb6r— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) August 4, 2020