Tuesday, August 4, 2020

Amnesty yaishutumu polisi ya Marekani

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeishutumu polisi nchini Marekani kwa uvunjaji wa haki za binadamu za waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.

Katika ripoti yake iliyochapishwa hii leo, shirika hilo linasema polisi ilitumia vurugu za kimwili mara kwa mara, kemikali kama vile gesi ya kutoa machozi na pilipili, pamoja na vitupo vingine visivyo na madhara makubwa kama risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji wa amani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, matukio ya hivi karibuni yamezusha wasiwasi kuhusiana na haki za kuishi, usalama wa mtu, ulinzi sawa wa sheria, uhuru wa kutobaguliwa na uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani.

Shirika hilo la haki za binadamu limeorodhesha matukio huru 125 ya matumizi ya nguvu isivyo laazima katika majimbo 40 pamoja na mji mkuu Washington.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...