Monday, June 1, 2020

Watumishi wa afya 7 wapata corona Uganda

Wizara ya Afya imesema watumishi 7 wa sekta ya afya nchini humo wamethibitishwa kupata maambukizi ya  COVID19

Waliopata Virusi hivyo ni Wauguzi 3, madaktari 2, na wafanyakazi 2 wa ngazi ya juu. Kwa mujibu wa Wizara, wamelazwa Hospitali na wanaendelea vizuri

Wataalam wapo katika maeneo mbalimbali ambapo watumishi wamekutwa na #COVID19 kuchunguza kilichopelekea wapate maambukizi

Hadi kufikia leo asubuhi,  Uganda imerekodi visa 417 vya Corona, huku waliopona wakiwa 72

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...