Monday, June 1, 2020
Donald TRUMP Muoga Sana... Akimbilia Chumba cha Chini ya ARDHI Baada ya Waandamanaji Kuidhingira IKULU Yote.....
Maandamano ya kupinga kuuawa kwa Mmarekani mweusi, George Floyd yamepelekea Washington DC kutangaza muda wa wananchi kubaki ndani baada ya Maandamano hayo kufanyika karibu na Ikulu (White House)
Kutokana na vurugu zilizokuwa zikiendelea nje ya White House, imeelezwa kuwa Usalama wa Taifa walimpeleka Rais Donald Trump kwenye chumba cha chini cha ardhi (Bunker) ambacho kilitumika wakati wa mashambulio ya kigaidi zamani
Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya waandamanaji zaidi ya 1,000 waliokuwa nje ya Ikulu na mabango huku wakiimba na kuwasha moto. Tangu kuanza kwa maandamano, inadaiwa takriban watu 4,100 wamekamatwa kutokana na makosa ya kuvunja maduka, kufunga barabara na kutozingatia muda wa kutotoka ndani
Mamlaka zimeweka zuio la muda wa kubaki ndani Washington DC pamoja na miji mingine mikubwa ikiwemo Atlanta, Chicago, Denver, Los Angeles, San Francisco na Seattle ili kudhibiti waandamanaji wanaopinga ukatili unaofanywa na Polisi mitaani
George Floyd alifariki dunia Jumatatu iliyopita huko Minneapolis baada ya Polisi mzungu, Derek Chauvin kumkandamiza shingoni kwa kutumia goti. Tangu tukio hilo, Chauvin pamoja na maafisa wengine watatu waliokuwepo wamefukuzwa kazi
Chauvin amefunguliwa mashtaka ya mauaji lakini waandamanaji wameendelea kudai hiyo haitoshi huku wakitaka Polisi wengine watatu waliokuwepo kushtakiwa
Source
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...