Wednesday, May 20, 2020

Uturuki yakemea vikali kuchomwa moto kwa bendera yake nchini Ugiriki

Uturuki kupitia msemaji wa wizara yake ya mambo ya  nje imekemea vikali kitendo cha kuchomwa moto bendera yake nchini Ugiriki.

Uturuki ikitaja kitendo hicho kuwa kitendo cha kibaguzi dhidi ya Uturuki  kilichofanywa na Ugiriki.

Hami Aksoy, msemaji wa zizara ya  mambo ya  nje ya Uturuki ameandika katika ukurasa wake wa Twitter akiwazindua wote wale ambao  hawajataba funzo  la athari za ubaguzi  na kukemea kitendo hicho cha kuchomamoto bendera ya Uturuki.

Hami Akasoy amekumbusha kuwa Baba wa Taifa la Uturuki Mustafa  Kemal Atatürk  hakuruhusu kukanyagwa kwa bendera ya Ugiriki iliokuwa chini ya miguu yake baada ya kuukomboa mjini Izmir  mwaka  1923 , mji ambao ulikuwa umekaliwa kimabavu na wagiriki.

Katika ujumbe wake , Hami Aksoy amesema kwa  Uturuki haitokubali bendera yake kudhalilishwa kama alivyofundisha Baba wa Taifa kwa kusemabendera ndio  heshima ya taifa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...