Friday, May 1, 2020
Ugonjwa Uliomuondoa Jaji Mkuu Mstaafu Ramadhani Huu Hapa, Leo Kuagwa Kitaifa Karimjee
Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ataagwa leo kitaifa katika viwanja vya vya Karimjee na mazishi yatafanyika kesho Kimara jijini Dar es Salaam.
Kiongozi huyo ataagwa kitaifa kwa mujibu wa sheria ya mazishi ya viongozi wa kitaifa ya mwaka 2006.
Taarifa iliyotolewa na msajili wa Mahakama ya Rufani, Kelvin Mhina jana ilieleza kuwa taratibu za mazishi na maandalizi zinafanywa na kusimamiwa na kamati ya mazishi ya viongozi wa kitaifa inayoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
'Siku ya Ijumaa (leo) kutakuwa na mazishi ya kitaifa viwanja vya Karimjee kuanzia saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana," ilieleza taarifa hiyo.
Aidha, Mhina alisema Jaji Ramadhani atazikwa kesho Jumamosi katika eneo la Makaburi ya familia yaliyopo Kimara King'ongo jijini Dar es Salaam.
Mazishi yatafanyika saa tisa alasiri na kutanguliwa na ibada itakayofanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano kuanzia saa 6:00 mchana jijini.
Jaji Ramadhani alifariki dunia Aprili 28, 2020 majra ya saa 2:05 asubuhi katika hospitali ya AgaKhan jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya saratani na mwishoni kupata mshtuko wa moyo (Heart Attack).
Marehemu Jaji Ramadhani alianza kuugua mwaka 2011 na kugundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ambao alipatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali nje na ndani ya nchi. Hospitali alizotibiwa ni Apolo na Banglow nchini India, Afrika Kusini, Nairobi na Dar es Salaam.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...