Friday, May 15, 2020
Sekondari ya Mboga yamshukuru Jakaya Kikwete
UONGOZI wa shule ya sekondari ya Mboga Kijiji cha Mboga Kata ya Msoga Chalinze Bagamoyo Pwani, unamshukuru Mlezi wao Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, kwa kufanikisha ujenzi wa mabweni.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo George Mwakyaba alitoa pongezi hizo shuleni hapo, akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwa sasa shule inaendelea na utoaji wa elimu, kutokana na ujenzi wa jengo la Maktaba kutoka kwa mlezi wao huyo.
Alisema kwamba Kikwete baada ya kubaini upungufu wa Maktaba, alijenga jengo moja lenye vyumba vitatu kikiwemo chumba kimoja kinachotumika kwa ajili ya Maabara, ambapo alitoa kiasi cha shilingi milioni 64 kwa ajili ya ujenzi huo.
"Kiasi hicho cha fedha ziliwezesha jengo hilo kufikia hatua ya kupauliwa, ambapo halmashauri ya Chalinze ilitupatia shilingi milioni 70, ambazo zilikamilisha majengo hayo matatu, kabla ya Wentwoth kuja kuyaboresha na kuwa ya kisasa zaidi," alisema Mwakyaba.
Aliongeza kuwa tangu shule hiyo iwe chini ya ulezi wa Rais Mstaafu, imekuwa katika mazingira bora ya majengo sanjali na ufundishaji, kwani walimu na wanafunzi wanafurahia mandhari yaliyopo shileni hapo, kwa kuwa na Maktabaa ikiwemo Maabara.
Katika shule hiyo mbali ya majengo hayo na madarasa ya kisasa, pia kuna nyumba za walimu zilizojengwa kuzunguka shule, ambazo zimeongeza kupendezesha eneo lote la shule, hali inayochangia kuwepo kwa amani kubwa shuleni hapo.
Akizungumzia mchango wa taasisi ya Wenthwoth kuhusu uboreshaji wa Maktaba na kompyuta, Mwakyaba aliishukuru taasisi hiyo kusaidia kompyuta 5, vitabu zaidi ya elfu moja na taulo za kike.
"Tunamshukuru Rais Mstaafu kwa kusaidia ujenzi pamoja na halmashauri yetu, pia taasissi ya Wentworth kwa kukarabati majengo hayo na kukabidhi konpyuta, internet na elimu ya matumizi ya mtandao ikiwemo mataulo kwa wanafunzi wa kike," alimalizia Mwalimu huyo.
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
