Kiongozi wa muda mrefu nchini Burundi Pierre Nkurunziza leo amempongeza mrithi wake aliyemteua kwa ushindi mkubwa aliopata katika uchaguzi wa rais, licha ya kuwa upinzani umeapa kuyapinga matokeo hayo mahakamani.
Maafisa wa uchaguzi walimtangaza Evariste Ndayishimiye , jenerali wa zamani wa jeshi aliyeteuliwa na chama tawala cha CNDD FDD kuwa mrithi wa Nkurunziza, kuwa mshindi wa uchaguzi wa Mei 20 kwa kupata asilimia 68.72 ya kura.
Nampongeza sana rais mteule jenerali Evariste Ndayishimiye kwa ushindi wake mkubwa ambao unathibitisha kuwa idadi kubwa ya Warundi wanakubali miradi na maadili aliyoianzisha, Nkurunziza ambaye aliamua kutowania kiti hicho baada ya miaka 15 madarakani, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter.
Mgombea wa upinzani Agathon Rwasa, amekuwa wa pili akipitwa kwa mbali amepata asilimia 24.19 ya kura, lakini chama chake cha National Freedom Council CNL, kimeyakataa matokeo hayo, kikidai kuwapo na udanganyifu katika uchaguzi huo.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
