Friday, May 8, 2020

Chadema yataka Kujua Kifungu Gani cha Sheria Kilichotumiwa Kuwaita Wabunge Kuhojiwa Polisi

Chadema

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amehoji ni kifungu gani cha sheria kilichotumika kuwataka wabunge waliopo mkoa wa Dar es Salaam kuripo polisi kwa ajili ya mahojiano.

"Afande barua nyingine zote wito huwa mnanukuu vifungu vya sheria mnavyovitumia kutoa wito husika. tamko hili halionyeshi vifungu hivyo kulikoni?,"

Mrema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa "Kuna ambao wako na familia, wengine karantini, wagonjwa wapo kwenye clinic zao, wengine kwa mujibu wa katiba,"
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...