Friday, May 8, 2020

China yakaribisha kujiunga na ubunifu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kupambana na Corona


Serikali ya China imekaribisha kujiunga na ubunifu wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya kukabiliana na virusi hatari vya Corona.

Hua Chunying, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema kwamba serikali ya Beijing inakaribisha kujiunga na ubunifu wa ushirikiano wa kimataifa wa WHO kwa ajili ya kuharakishwa utafiri na uzalishaji wa vifaa vya afya vinavyohusiana na virusi vya corona


Chunying ameongeza kwamba serikali ya China inaunga mkono nafasi ya Shirika la Afya Duniani katika mapambano yake dhidi ya Corona na hivyo inakaribisha na kushiriki katika ubunifu na mapendekezo ya shirika hilo kwa lengo la kuharakisha shughuli za kufanyika utafiti, uzalishaji na kugawa chanjo na dawa za kukabili virusi vya Corona. Kabla ya hapo, Tedros Adhanom Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani alitangaza kuzinduliwa ubunifu wa ushirikiano wa kimataifa huku akionyesha matumaini kwamba China itajiunga na mpango huo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...