Sunday, May 31, 2020

Njia ya kutunza mayai kwa njia ya asili

Kwa kawaida kuku huanza kutetea (Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano.

Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20.

Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.

Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.

Uatamiaji wa mayai na uanguaji wa vifaranga
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni – Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili

Kuchagua mayai ya kuangua.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

Kumtayarisha kuku wa kuatamia
Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.

Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
Pia mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
Weka mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.

Ni vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.

Pia jifunze mbinu za kuatamia mayai mengi kwa njia za asili.
Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na kutotoa pamoja.

Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.
Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia.

Mwekee mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.

Utekelezaji wake.

Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku anayotaga.

Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.

Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10

Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.

Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya ukweli wakati wa usiku.

Muhimu.
Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya taa, manukato n.k.

Jifunze pia kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasuyo na mbegu.



Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au kuyauza.

VIDEO: IGP Sirro awaonya wanaotoka jela kwa misamaha "wasilaumu serikali"


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka baadhi ya wananchi ambao ni washtakiwa au wafungwa wanaopata msamaha wa Rais kutoka gerezani, kuacha kujiingiza katika matukio ya uhalifu jambo ambalo nikinyume na sheria za nchi. 

IGP Sirro amesema hayo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi mkoani Singida ambapo alizungumza na Polisi Kata waliopo kwenye mkoa huo na kuwataka kuendelea kushirikiana na wananchi katika mapambano dhidi ya uhalifu ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu hususan wa kutumia silaha za moto. 

Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, wenyeviti wa kamati za Ulinzi na usalama za wilaya na mikoa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kwamba hadi kufikia sasa hali ya usalama nchini imeendelea kuwa shwari.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Awamu ya Pili Ya Watanzania Waliokwama India Warejea Nchini

Serikali yarejesha kwa awamu ya pili Watanzania 192 waliokuwa wamekwama nchini India kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19

Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Tanzania [ATCL] pamoja na Diaspora wa Tanzania nchini India kwa mara nyingine wamefanikisha safari ya pili ya kuwarejesha nchini Watanzania 192 waliokuwa wamekwama katika miji mbalimbali nchini India.

Watanzania hao walikwama kutokana na zuio la kuingia na kutoka kwa ndege za Kimataifa lililowekwa na Serikali ya India kama hatua mojawapo ya kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Ndege maalum ya aina ya Boeng 787-8 ya Dreamliner ya Shirika la Ndege la Tanzania ilitumwa tena na Serikali Jijini Mumbai kuja kuwachukua Watanzania hao waliokwama nchini India tangu tarehe 22 Machi 2020 lilipowekwa zuio hilo na Serikali ya India.

Ndege hiyo iliondoka tarehe 30 Mei 2020 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji,  Mumbai ikiwa imebeba jumla ya raia wa Tanzania 192, miongoni mwao ni waliokuwa wamekwenda India kwa ajili ya matibabu; wahitimu kutoka vyuo mbali mbali na wanafunzi ambao wanalazimika kurudi nyumbani kwa kuwa vyuo vimefungwa hadi mwezi Agosti/Septemba 2020.

Tofauti na awamu ya kwanza, safari hii pia ilihusisha kuwarejesha nchini India raia wa nchi hiyo wapatao 202 ambao walikuwa wamekwama nchini Tanzania. Hatua hii ya Serikali ya Tanzania itasaidia sana katika kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya India na Tanzania.

Mpaka sasa jumla ya Watanzania 438 wamerejeshwa Tanzania kutoka India kwa utaratibu huu maalum.

Rwanda yaripoti kifo cha kwanza cha ugonjwa wa Corona

Wizara ya Afya ya Rwanda imetangaza kifo cha kwanza kilichosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 (corona) katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Katika taarifa ya leo Jumapili, wizara hiyo imesema aliyeaga dunia ni dereva wa lori mwenye umri wa miaka 65 na ambaye alikuwa amerejea nchini humo hivi karibuni kutoka nchi jirani ambako alikuwa anaishi.

Taarifa hiyo imesema mtu huyo ameaga dunia akipokea matibabu katika moja ya vituo maalumu vya kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Rwanda, watu 359 wameambukizwa virusi vya corona nchini Rwanda kufikia jana Jumamosi ya Mei 30. Aidha idadi ya wagonjwa wa corona waliopata ahueni nchini humo imeongezeka na kufikia watu 250.


Serikali Yatahadharisha Tegesha Nyamongo

Na Munir Shemweta, WANMM TARIME
Serikali imewatahadharisha wananchi wa kijiji cha Komarera kata ya Nayamongo Tarime Vijijini mkoani Mara kuacha tabia ya kufanya maendelezo maarufu kama Tegesha katika eneo linalotaka kuchukuliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara kwa shughuli za uchimbaji madini.

Tahadhari hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki Nyamongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara na Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha wakati wa kutangazwa notisi ya kusitisha kufanyika maendelezo kwenye vijiji vinavyozunguka Mgodi wa North Mara vya Kemorera na Kewanja vilivyopo wilayani Tarime na Mkuu wa wilaya Mtemi Msafiri.

Evelyne alisema, wakati mchakato wa kutwaa eneo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini ukifanyika tayari baadhi ya wananchi wasio waaminifu katika maeneo ya Nyamongo wameanza kufanya maendelezo kwa kasi (Tegesha) kwa kupanda migomba na Mialovela lengo likiwa kujipatia fedha wakati wa zoezi la uthamini.

''Wananchi mmekosa subira kabisa mmeanza kupanda mialovera, migomba, miembe  na katani ili mjipatie fedha huko ni kutegesha na serikali haiko tayari kuwalipa watu wa aina hiyo, mimi kama mshauri wa uthamini nasema ni kosa kufanya hivyo'' alisema Evelyne

Amewataka wananchi wa wameneo hayo hasa wanawake kutodanganywa kwa kushiriki kupanda vitu kwa kutegesha kwa kuwa havitahesabiwa na badala yake wote waliofanya hivyo waondoe walivyoapanda ili kuepuka hasara ya kutolipwa.

Akitangaza uamuzi wa kusitisha maendeleo kwenye eneo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Injinia Mtemi Msafiri alisema kuanzia siku ya kutangazwa notisi ya usitishaji hairuhusiwi mtu yoyote kufanya maendelezo na wananchi ambao vijiji vyao vinapitiwa na zoezi hilo wanatakiwa kusubiri zoezi la uthamini na atakayeenda kinyume atahesabika kama ametegesha

Alisema, Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara sasa unamilikiwa kwa ubia wa Kampuni ya Barick na Serikali kupitia Twiga Corporation Ltd na kusisitiza udanganyifu utakaofanyika utasababisha wananchi kutolipwa kwa wakati kama ilivyotokea kwenye zoezi la awali lililolazimu kufanyika uhakiki katika maeneo yaliyothaminiwa.

Kwa mujibu wa Mrakibu wa Maendeleo ya Jamii wa Mgodi wa Barrick North Mara Sadala Hamis eneo linalotakiwa kuchukuliwa kwa shughuli za uchimbaji madini kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo lina ukubwa wa takriban hekta 404 na wakazi wasioopungua mia tatu.

Hivi karibuni wakati wa kutoa fidia ya shilingi bilioni 33 kwa wakazi 1,639 wa vijiji vya Matongo na Nyabichune katika eneo la Nyamongo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazo Dkt Angeline Mabula alieleza kuwa zoezi la utoaji fidia lilichukua muda mrefu kwa sababu wananchi hawakuwa wakitoa taarifa sahihi na baadhi kutegesha na kuwaasa kutoa ushirikiano na kuwa wakweli katika masuala yanahusu ulipaji fidia sambamba na  kuwataka kutowekeza maeneo ambayo mgodi unataka kuyachukua.

Bosi wa AC Milan apinga kuanza kwa Coppa Italia

Rais wa klabu ya AC Milan, Paolo Scaroni amesema anapinga mpango wa kuanza kwa mechi za nusu fainali na fainali za kombe la Coppa Italia katika kipindi hiki ambacho michezo inatarajiwa kurejea upya kufuatia kusimamishwa tarehe 9 mwezi Machi mwaka huu kwa hofu ya mlipuko wa janga la virusi vya Corona.


Waziri wa michezo nchini Italia, Vincenzo Spadafora alithibitisha siku ya Alhamis kuwa ligi ya Serie A huenda ikarejea tena tarehe 20 mwezi Juni huku michezo ya kombe la Coppa Italia ikitarajiwa kuanza Juni 13 kwa mechi ya Napoli dhidi ya Inter Milan na Juventus ikiwavaa AC Milan, na fainali kupigwa siku tatu badae.

"Tunatambua thamani ya kuweza kuonyesha mechi zote katika ubora baada ya miezi kadhaa ya kusimamishwa kwa mchezo wa soka," Scaroni aliliambia shirika la habari la ANSA.

"Lakini, kwa mtazamo wa michezo, tunaona kuwa ni muhimu tukabuni mechi mbili kwa siku tatu baada ya zaidi ya miezi mitatu ya mapumziko."

Gazeti la dello Sport lilinukuliwa kwa kusema kuwa Inter Milan na Juventus pia walikuwa wanapingana na mipango hiyo.

Marais wengine wawili wa klabu waliridhia uamuzi wa serikali wa kuanza tena msimu mpya.

"Ninauhakika kuwa kwa kuanza tena hatua hii, mpira wetu wa miguu utaweza kudumisha kiwango hicho cha hali ya juu ambacho kinatambulika kote ulimwenguni,"alisema Claudio Lotito Rais wa Lazio, ambaye timu yake inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya  Serie A, wakiwa nyuma ya alama moja dhidi ya vinara, bibi kizee wa Turin, Juventus.

Gari Aina ya TOYOTA Harrier Inauzwa Bei Nafuuu..Lipo Dar es Salaam Mbezi Beach




Gari aina ya Toyota Harrie ya Mwaka 2006
Plate number: DHE
Imetembea Kilometre 66,697 tu
Upo Dar es Salam, Mbezi Beach
Halina tatizo lolote 
Bei Milioni 19 .5 

Maelewano Kidogo Yapo

Piga simu 0714604974 Kwa Maelezo zaidi na kutaka kuliona gari








Source

Saturday, May 30, 2020

Lwakatare: Rasmi Arudi CUF

WILFRED Lwakatare, Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia Chadema, amekwenda kinyume na kiapo cha kustaafu siasa, kwa kurudi katika Chama cha Wananchi (CUF), alichokuwepo awali.

Mara kadhaa Lwakatare alitangaza kustaafu siasa, ambapo  tarehe  14 Aprili 2020, akiwa bungeni jijini Dodoma, alisema hana mpango wa kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020, na wala hatojiunga na chama chochote cha siasa.

Lakini leo Jumamosi tarehe 30 Mei 2020, Lwakatare amerudi CUF na kupokelewa na Maftah Nachuma, Makamu Mwenyekiti wa CUF Bara, katika Ofisi Kuu za chama hicho, zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam.

Lwakatare amerudi CUF baada ya kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kosa la kukaidi agizo la chama hicho, lililowataka wabunge wake kutohudhuria vikao vya bunge kwa muda wa siku 14.

Chadema kiliwataka wabunge wake  wajiweke karantini kama tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19).

Akitoa sababu za kwenda kinyume na msimamo wake wa kustaafu siasa, Lwakatare amesema CUF kilimuomba arudi.

 "Miaka mitatu, nilitangaza wazi hata bungeni wanafahamu nikasema mimi natarajia ifikapo Oktoba 2020 nikimaliza kipindi cha Bunge sigombei tena nataka nipumzike ili nifanye mambo mengine. Mungu ana muda wake. Nimebakiza mita chache kumaliza mbio nashtukia leo nimeinuliwa tena," amesema Lwakatare.

Sambamba na hilo, Lwakatare amesema yeye ni miongoni mwa watu waliokiasisi chama cha CUF, hivyo amerudi ili kuhakikisha chama hicho kinaimarika, hususan kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 2020.

Akizungumzia kuhusu hatma ya ubunge wake, Lwakatare amesema yeye ni mbunge anayetambuliwa na Ofisi ya Spika wa Bunge, baada ya chama chake kumfukuza.

"Mimi nimetoka Chadema, ni mbunge anayetokana na ofisi ya spika sababu mimi chama changu kimenifukuza. Najidai sina deni na mtu, siangalii kushoto wala kulia," amesema Lwakatare.

Lwakatare ameahidi kutumia uzoefu wake katika masuala ya uchaguzi, katika kuhakikisha CUF, kinapata ushindi.

"Mimi ni mtaalamu wa uchaguzi, nimegombea chaguzi nimeshinda na nimeshindwa . Sijawahi kushindwa kwa kura za aibu, lakini nikishinda nashinda kwa kishindo. Sikwepeshi Chadema wananijua, CCM  wananijua na hata CUF mnanijua," amesema Lwakatare na kuongeza:

"Uchaguzi ni namba, ukipoteza mtu mmoja umepoteza kundi kubwa la watu. Sio sifa kuwa mpinzani siku zote."

Wakati huo huo, Lwakatare ametoa msimamo wake kuhusu utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akisema kwamba ili itende haki, wanatakiwa kuja mbinu zitakazowawezesha kukwepa changamoto cha tume hiyo.

Miongoni mwa changamoto zinazolalamikiwa na vyama vya upinzani dhidi ya utendaji wa NEC, kutotangazwa kwa washindi halali wa uchaguzi.

Lwakatare amesema, yeye ana mbinu za kushinda changamoto za NEC, ndiyo maana ameweza kutangazwa mbunge na tume hiyo kwa zaidi ya mara moja, pindi aliposhinda kwenye uchaguzi.

"Sisi tumekuja bungeni si chini ya mara moja, kwa tume hii tuliyo nayo. Tuulizeni tulishindaje, tuulizeni tulitumia mbinu zipi?.  Ili anayekuja kugombea ajue mbinu na kuacha kulia kwamba tume hii sio huru," Wilfred Lwakatare, Mbunge Bukoba Mjini.

Lwakatare amesema, wanasiasa wanaolalamika kuibiwa kura katika uchaguzi, ni wazembe.

"Maalim Seif huko Zanzibar kila siku anasema anaibiwa kura, hamjui kuibiwa ni udhaifu?  Kama uko makini na unajitambua huwezi kuibiwa,  kuibiwa ni sehemu ya uzembe na unyonge wa kutojua kuingia kwenye uchaguzi," amesema Lwakatare.

Source

Nyalandu asilimulia mazito baada ya watu kutelekeza gari kwenye geti lake, asema anaelewa kinachoendelea


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, asimulia jinsi gari lenye alama ya kampuni ya simu ya mkononi tigo lilivyotekelezwa kwenye geti la nyumba yake.

Nyalandu amesema baada ya gari hilo kutekekezwa majira ya asubuhi wahusika waliondoka.

"Gari yenye usajili wa @tigo-GT#T562 DRS lilipakiwa ndani ya Entrance gate ya nyumbani kwangu na wahusika wakaliacha na kuondoka mapema asubuhi ya leo," aliandika Nyalandu katika ukurasa wake wa Twitter.

"@tanpol kupitia OCD wa Arusha wanakuja kuchunguza mkasa huu na majirani wamejitolea kutoa ulinzi wakati tunajua kilichojiri,"

Corona: Korea Kusini yafunga shule tena baada ya maambukizi kuongezeka zaidi

Zaidi ya shule 200 nichini Korea Kusini zimelazimika kufunga tena shule siku chache baada ya kufunguliwa, kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Mapema Jumatano, melfu ya wanafunzi walirejea shuleni baada ya kufunguliwa tena nchini humo na kulegeza masharti yaliyowekwa awali kukabiliana na virusi vya corona .

Lakini baada ya siku moja tu, maambukizi mapya 79 yalirekodiwa, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kwa siku nchini humo kwa kipindi cha miezi 12.

Maambukizi haya mapya yalihusisha watu wa kituo kimoja ambacho kipo nje ya mji wa Seoul.

Ghala ambalo lililopo mji wa Bucheon, linaloendeshwa na kampuni kubwa ya kibiashara ya Coupang, na maafisa wanasema sehemu hiyo ilikuwa haitekelezi kikamilifu hatua za kuzuia maambukizi.

Maafisa wa afya walibaini maambukizi ya virusi vya corona katika viatu na mavazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Inawezekana Korea Kusini ikaendelea kurekodi maambukizi mapya wakati huu inapoendelea kupima maelfu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Maambukizi mapya 58 yalirikodiwa siku ya Ijumaa, na kusababisha taifa hilo kuwa na jumla ya idadi ya watu wenye maambukizi ya corona 11,402.

'Kitovu cha maambukizi'

Jumla ya shule 251 huko Bucheon zimelazimika kufungwa .

Imeripotiwa katika gazeti la Korea Times, kuwa Wizara ya Elimu imesema jumla ya shule 117 katika mji mkuu wa Seoul pia zimeahirisha tarehe ya kufunguliwa tena kwa shule.

Mwanafunzi mmoja mjini Seoul ambaye mama yake alikuwa akifanyakazi katika ghala la kampuni ya Coupang pia naye amepatikana na na virusi vya corona.

Taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya Rais-IKULU




Video Mpya : PILI NZALIA - MACHIMBO


Hii hapa ngoma mpya ya Pili Nzalia inaitwa Machimbo...
itazame hapa

POLISI ALIYEMUUA KIKATILI MMAREKANI MWEUSI ASHITAKIWA KWA MAUAJI YA BILA KUKUSUDIA


Afisa wa polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya kikatili ya  Mmarekani mweusi, George Floyd ametiwa mbaroni na kushtakiwa kwa kosa la mauaji   kufuatia kifo cha Raia huyo mweusi ambaye alimuua kwa kumkanyaga shingo na kumfanya akose pumzi.

Hayo yanatokea katika kipindi ambacho mamlaka nchini  humo zimetangaza marufuku za kutotoka nje baada ya vurugu za maandamano ya siku tatu ambazo zimesababisha baadhi ya maeneo kuchomwa moto. 

Derek Chauvin, afisa wa polisi mzungu ambae alichukuliwa video, ikionesha kambana kwa kutumia goti shingoni, marehemu George Floyd kwa karibu dakika tisa, anashitakiwa kwa kusababisha kifo pasipo kukusudia


Friday, May 29, 2020

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, ambapo walijadili masuala mbalimbali yanayohusu mahusiano baina ya Tanzania na Italia.

Aidha, walitumia mazungumzo hayo kujadili hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Serikali ya Italia katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19.

Mhe. Waziri alifahamisha kuwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kwenye
mapambano ya ugonjwa huo zimezingatia mazingiria na hali halisi ya Tanzania pamoja na nchi jirani zinazozunguka Tanzania.

Kwa upande wake Balozi Mengoni alipongeza juhudi hizo za Serikali ambapo alifahamisha kuwa Serikali yake ya Italia inaziunga mkono na kwamba ipo tayari kutoa ushirikiano pale itakapohitajika kufanya hivyo.


Viongozi hao walikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya Mataifa hayo mawili ambao umejikita katika sekta za elimu, afya, utalii pamoja na biashara na uwekezaji

Walinzi wa amani 500 wapelekwa Minnesota na St. Paul

Wanajeshi 500 wa kikosi cha ulinzi wa taifa pamoja na wanajeshi wa anga wamesambazwa kwenye miji ya kaskazini mwa Marekani ya Minnesota na St. Paul baada ya siku tatu za maandamano ya vurugu, kufuatia kifo cha mmarekani mweusi George Floyd.

Meja Jenerali wa jeshi Jon Jensen wa kikosi cha walinzi hao cha Minnesota amesema wanajeshi waliosambazwa wana mafunzo ya kuwalinda raia, mali na kuhakikisha haki ya watu kuandamana kwa amani.

Hatua hiyo ilianza usiku wakati waandamanaji walipoanza kupora na kuchoma majengo kadhaa kote kwenye miji hiyo, kufuatia ghadhabu zilizochochewa na ukatili wa polisi dhidi ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika.

Wanajeshi hao watasaidia polisi wa miji hiyo kulinda amani kuanzia leo.

Picha : WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAPATIWA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA...MWENYEKITI SPC ATAKA WACHUKUE TAHADHARI

Na Damian Masyenene - Shinyanga Press Club
Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga(SPC) imegawa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya homa kali ya mapafu Corona kwa waandishi wa habari,ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao katika mazingira salama na kuepuka maambukizi.

Vifaa walivyopewa wanachama ni barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni za maji 'Hand soaps' ambapo zoezi la ugawaji vifaa hivyo limesimamiwa na Viongozi wa SPC wakiongozwa na Mwenyekiti wa SPC Kadama Malunde kwa waandishi wa habari waliopo Shinyanga Mjini  na Makamu Mwenyekiti wa SPC, Shaban Alley kwa waandishi wa habari waliopo Kahama Mjini.

Akigawa vifaa hivyo leo Mei 29 kwa wanachama wa SPC ,Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde amesema kuwa,vifaa hivyo vimetolewa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania kwa wanachama wake kuwakinga na virusi vya Corona.

Malunde amewataka waandishi wa habari kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata masharti na miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya.

Malunde amesema kila mwandishi ambaye ni mwanachama wa SPC amepata barakoa nne, sabuni ya kunawia moja, vitakasa mikono viwili na gloves tatu,huku akiwaomba wadau wengine kusaidia waandishi wa habari vifaa vya kujikinga na Corona kwa kuwa ni kundi ambalo linakutana na watu wengi.

"UTPC iliona ni vyema kuwapatia vifaa waandishi wa habari kwani ni kundi ambalo linakutana na watu mbalimbali na huwezi kujua ni nani ana virusi vya Corona,ndiyo maana tumegawa vifaa hivyo viweze kuwasaidia wanapokuwa kazini",amesema Malunde.

Nao baadhi ya waandishi wa habari wameishukuru UTPC kwa kutoa vifaa hivyo kwa waandishi wa habari kupitia kwenye Klabu za waandishi wa habari kwani vitakuwa ni msaada mkubwa katika kazi zao katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya Corona.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni za maji 'Hand soaps' kwa ajili ya waandishi wa habari leo Ijumaa Mei 29,2020. Kushoto ni Mweka Hazina wa Shinyanga Press Club, Stella Ibengwe. Picha na Shinyanga Press Club
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kujikinga na Corona kwa waandishi wa habari ambapo amewasisitiza kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu Ugonjwa huo.
Muonekano wa vifaa vya kujikinga na Corona vilivyotolewa kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Awali Mratibu wa Shinyanga Press Club, Estomine Henry (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa SPC, Kadama Malunde kabla ya kuanza kugawa vifaa hivyo kwa wanachama wa SPC

Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni  Mweka Hazina wa Shinyanga Press Club, Stella Ibengwe ambaye ni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi.
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Radio Faraja, Moshi Ndugulile.
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Radio Faraja, Mc Donald Masse.
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera, Amos John.
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Damian Masyenene.
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habarileo, Kareny Masasy.
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa  Radio Faraja, Stephen Kanyefu.
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Radio Free Africa, Shangwe Than.
Mwandishi wa habari wa Radio Free Africa, Shangwe Than akizungumza jambo wakati akipokea vifaa vya kujikinga na COVID - 19.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira Suleiman Abeid.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe, Marco Maduhu.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) , Kadama Malunde akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Sam Bahari.
Sehemu ya wanachama wa Shinyanga Press Club Mjini Shinyanga wakiwa na vifaa vya kujikinga na COVID -19.
Sehemu ya wanachama wa Shinyanga Press Club Mjini Shinyanga wakiwa na vifaa vya kujikinga na COVID -19.

KAHAMA: Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) Shaban Alley akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni  Katibu wa Shinyanga Press Club, Ally Lityawi ambaye ni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima.
Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) Shaban Alley akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni  Katibu wa Shinyanga Press Club, Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira, Patrick Mabula.
Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) Shaban Alley akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni  Katibu wa Shinyanga Press Club, Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Salvatory Ntandu.
Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) Shaban Alley akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni  Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe, Neema Sawaka.
Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) Shaban Alley akimkabidhi vifaa vya kujikinga na COVID -19 ikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni  Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe, Shaban Njia.
Wa Kwanza kushoto ni Mwandishi wa Radio Huheso Fm, Chevawe Mandari,akifuatiwa na Neema Sawaka wa Gazeti la Nipashe,Othman Nyamiti wa Divine Fm, Shaban Alley wa Star Tv, Ally Lityawi wa Gazeti la Tanzania Daima na Paul Kayanda wakiangalia vifaa kwa ajili ya kujikinga na COVID -19 zikiwemo barakoa (masks), vitakasa mikono (sanitizers), medical gloves na sabuni. 
Sehemu ya Wanachama wa Shinyanga Press Club waliopo Kahama Mjini wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kupokea vifaa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya COVID -19.
Sehemu ya Wanachama wa Shinyanga Press Club waliopo Kahama Mjini wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kupokea vifaa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya COVID -19.
Picha na Shinyanga Press Club
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...