Sunday, May 31, 2020

Bosi wa AC Milan apinga kuanza kwa Coppa Italia

Rais wa klabu ya AC Milan, Paolo Scaroni amesema anapinga mpango wa kuanza kwa mechi za nusu fainali na fainali za kombe la Coppa Italia katika kipindi hiki ambacho michezo inatarajiwa kurejea upya kufuatia kusimamishwa tarehe 9 mwezi Machi mwaka huu kwa hofu ya mlipuko wa janga la virusi vya Corona.


Waziri wa michezo nchini Italia, Vincenzo Spadafora alithibitisha siku ya Alhamis kuwa ligi ya Serie A huenda ikarejea tena tarehe 20 mwezi Juni huku michezo ya kombe la Coppa Italia ikitarajiwa kuanza Juni 13 kwa mechi ya Napoli dhidi ya Inter Milan na Juventus ikiwavaa AC Milan, na fainali kupigwa siku tatu badae.

"Tunatambua thamani ya kuweza kuonyesha mechi zote katika ubora baada ya miezi kadhaa ya kusimamishwa kwa mchezo wa soka," Scaroni aliliambia shirika la habari la ANSA.

"Lakini, kwa mtazamo wa michezo, tunaona kuwa ni muhimu tukabuni mechi mbili kwa siku tatu baada ya zaidi ya miezi mitatu ya mapumziko."

Gazeti la dello Sport lilinukuliwa kwa kusema kuwa Inter Milan na Juventus pia walikuwa wanapingana na mipango hiyo.

Marais wengine wawili wa klabu waliridhia uamuzi wa serikali wa kuanza tena msimu mpya.

"Ninauhakika kuwa kwa kuanza tena hatua hii, mpira wetu wa miguu utaweza kudumisha kiwango hicho cha hali ya juu ambacho kinatambulika kote ulimwenguni,"alisema Claudio Lotito Rais wa Lazio, ambaye timu yake inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya  Serie A, wakiwa nyuma ya alama moja dhidi ya vinara, bibi kizee wa Turin, Juventus.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...