Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema watu watano wanashikiriwa na jeshi hilo kwa tuhuma za mauaji ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chilungulu, Wilaya ya Bahi, Eradius Mgaya(41) na kumtupa kwenye shamba la shule.
Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari Jijini Dodoma, ,amesema tukio hilo lilitokea Aprili 7, mwaka huu katika kijiji cha Chilungulu.
Muruto amesema kuwa Mwalimu huyo alipigwa na kitu chenye ncha kali na kutupwa kwenye shamba la shule hiyo.
"Hawa watuhumiwa walimvizia njiani alipokuwa akirejea nyumbani kwake, jeshi la polisi bado tunachunguza chanzo cha kifo na watuhumiwa tunawashikilia hadi hapo tutakapokamilisha uchunguzi,"ameleza Muruto.
Katika hatua nyingine, Mkazi wa Image jiji la Dodoma Godfrey Shirima (22) anashikiliwa kwa kukutwa na silaha aina ya Bastola yenye namba za usajili 016975 ambayo anamiliki kinyume na sheria huku akiitumia katika uhalifu.
Hata hivyo,Muruto amesema kuwa mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika.
Muroto hakutaja majina ya watuhumiwa hao na kudai kwamba bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.
Wakati huo huo, Kamanda huyo ameonya mikusanyiko isiyo ya lazima itakayosababisha msongamano hasa wakati huu ambapo kila raia anapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
"Nitoe rai kwa Wazazi kuwalinde watoto wao na wasiwaruhusu kwenda kwenye mikusanyiko kama ilivyozoeleka, pia watu wajiepushe na ulevi wa kupindukia na kuchukua tahadhari ya usalama barabarani,"Muroto ametoa wito.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
