Tuesday, April 14, 2020
UNAJUA Kwanini Mapenzi ya Mbali Hayadumu? Hizi Hapa Sababu 5..!!!
Wengi wetu hujiuliza kwanini maisha ya mapenzi ya mbali huwa hayafiki mbali na kubaki wa kijiuliza tatizo ni nini? Wakati mwingine watu huanza kuulizanaa mchawi ni nani katika mapenzi yao. Laa hasha!! Huenda mchawi wa mapenzi yako ni wewe mwenyewe lakini hujui kwa sababu hakuna mtu ambaye ameshawahi kukueleza jambo hili na lile ndio tatizo
Hata hivyo hakuna kumbukumbu ambazo zinaonesha ni kwa asilimia ngapi ambazo wapenzi wanapenda kuwa mbali mbali japo mazingira mara nyingi ndo huwa chanzo
Katika tafiti mbali mbali zinaonesha kwamba umbali humaliza kabisa mapenzi ambayo wapenzi wengi wenye malengo ya kufika mbali huwakuta.
Lakini zipo sababu mbalimbali ambazo ukizichanganua utajua kwa nini mapenzi mengi ya mbali huw hayadumu
Wivu.
Wivu huwa ni chachu ya kupima upendo lakini ukizidi pia huwa tatizo. Wivu wa mapenzi ukizidi husababisha kutokuaminiana kwani kila mmoja kwa wakati wake tofauti huhisi mwenzake anamsaliti, mara nyingi hali kama hii humfanya mmoja wapo kati ya wapenzi hao wawili kuona kama mwenzake ameshamchoka na anamtafutia sababu. Ni vyema kuwa na wivu kiasi kwa mpenzi wako
Mawasiliano
Mawasiliano huimarisha mapenzi na hufanya wahusika kujihisi wapo pamoja. Inapotokea kuwa na ufinyu wa mawasiliano ndipo hali ya mapenzi ya upande mmoja hupungua na kuhisi kwamba tayari mwanamke/mwanaume tayari ameshapata mwingine wakumfanya asifanye mawasiliano ya mara kwa mara.
Ugomvi
Magomvi ya mara kwa mara hufanya mmoja wenu ahisi kuchoka na mahusiano. Inapotokea sababu za ugomvi ambao unahisi unaweza kuwa chanzo cha kuvunja mahusiano yenu ni afadhali ukazizuia na kutafuta siku nyingine ya kutatua tatizo hilo.
Kutojali
Hii mara nyingi imetajwa sana kuwa ni chanzo cha mapenzi ya mbali kuvunjika kwa sababu tofauti mfano mpenzi wako alipokuwa karibu ulikuwa ukimpatia huduma mbalimbali kama zawadi nk, lakini anapokuwa mbali unajisahau hali hii humfanya mpenzi wako ajiulize kulikoni?
Usikivu
Nayo ni sababu ambayo ukiwauliza wengi wao ambao walikuwa na uhisiano wa mbali ukavunjika lazima atakulalamikia kwamba alikuwa hanisikilizi nachomwambia. Mfano alitaka kutoka kwenda 'OUT' na wenzake nikamyima lakini hajanisikiza hivyo hanifai.
Hizi huenda zikawa ni baadhi ya sababu ambazo wapenzi wengi ambao mapenzi yao hayajafanikiwa kama jinsi walivyo hitaji wamekumbana nazo.
Ili kuepuka changamoto za kutengana na mtu ambaye unamuhitaji katika maisha yako ni vyema ukaanza kujifunza pole pole kutoka kwake ili siku ukiwa mbali naye ujue kipi mwenzako anapenda na kipi hakipendi mnapokuwa mbali.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
