Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) itawahudumia wagonjwa wenye matatizo ya moyo yanayohitaji matibabu ya kibingwa walioko katika kituo cha watu waliopata maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID – 19) cha Amana jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof.Mohamed Janabi alipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kuona ni namna gani wataalamu wa Taasisi yake wataweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo.
Prof. Janabi alisema licha ya Taasisi hiyo kwenda katika kituo hicho kutoa huduma ya matibabu ya kibingwa ya moyo pia itatoa mafunzo kwa vikundi vya watu wachache kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo ambayo yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi wa kila siku hasa katika kipindi hiki cha janga la Corona.