Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kukamilisha mahitaji muhimu ya Hospitali ya Wilaya hiyo ambayo iko katika hatua za ukamilishaji wa ujenzi kwa tahadhari ya kupokea wagonjwa wa Korona endapo hali isipotengemaa.
Jafo ameyasema hayo mapema leo alipotembelea Hospitali hiyo inayojengwa katika eneo la Mlowo Wilayani Chamwino na kukuta ujenzi katika hatua za ukamilishaji kisha kutoa rai hiyo kwa viongozi kujiandaa mapema na Janga hili la Kidunia.
Amesema kutokana na Jiografia ya hospitali hii kuwa imejitenga kabisa na maeneo ya makazi ya watu ninashauri muandae jengo moja maalumu na mlikamilishe kwa kila kitu kinachohitajika ili endapo janga hili likiendelea jengo hilo litumika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa Korona.
"Kwa hali tuliyonayo sasa hatutakiwa kukaa kusubiria mpaka hali iwe mbaya zaidi tunatakiwa kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari za awali kabisa ikiwa ni pamoja na kuandaa maeneo ya kutolea huduma kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huu hatari na hospitail yetu hii naona inafaa kabisa kwa kuwa ina sifa zote" alisisitiza Jafo.
Wakati huo huo Waziri Jafo aliwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Chamwino kwa kusimamia kwa makini ujenzi wa Hospital hiyo na kuhakikisha kuwa inakamilika kwa ubora wa hali ya juu na kwa wakati.
"Nimefurahi kukuta ujenzi umefikia katika hatua hii ya ukamilishaji, vitu vidogo sana ndio vimebakia kumalizia kabisa ujenzi na majengo yote yanaonekana kuwa na ubora wa hali ya juu hakika nimefurahishwa na hatua hii na hongereni sana" Alisema Jafo.
Haya kwangu mimi naona kama ni mafanikio kwani mwanzoni hali ilikua mbaya, ujenzi ulikua unasuasua nilitumia nguvu kufuatilia na kusimamia lakini kwa sasa wote tunajivunia mafanikio haya huu ndio uongozi wa pamoja unaotakiwa katika utekelezaji wa miradi.
Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ni miongoni mwa HospitaIi za Halmashauri 71 zinazoendelea kujengwa Nchini Kote kupitia mpango wa Maboresho wa Huduma za Afya unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...




