Sunday, November 17, 2019

Waandamanaji 40 wakamatwa Iran

Watu 40 wamekamatwa katika mji wa Yazd nchini Iran baada ya kupambana na polisi wakati wa maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya petroli.

Taarifa hii ni kulingana na shirika la habari nchini humo la ISNA hii leo. Shirika hilo lilimnukuu mwendesha mashitaka wa serikali Mohammad Hadadzadeh akisema wale wanaoshikiliwa ni waliosababisha vurugu akiwatuhumu kwa matukio ya uharibifu na wengi miongoni mwao si wakaazi wa eneo hilo.

ISNA hata hivyo, haikuweka wazi ni wakati gani watu hao walikamatwa. Iran ilikabiliwa na maandamano makubwa siku ya Ijumaa masaa kadhaa baada ya tangazo la bei la petroli kupandishwa kwa asilimia 50 katika lita 60 za mwanzo na asilimia 300 kwa kiasi chochote kitakachozidi kila mwezi.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...