Friday, August 30, 2019
Harmonize Huu ni muda wa kuungana Na Clouds (CMG),Utafika mbali Bro.
Hey Guys...
I Hope mko poa wakubwa,,,Ryt,,??
Okay Fresh
Najua watu wengi nikiwemo Mimi wanajiuliza,Je Ngoma za Harmonize zitaanza kupigwa Clouds baada ya kujitoa kwenye lebo ya hasimu wao?
Hilo swali wengi hatuna majibu.
Nakumbuka kipindi bifu la Diamond na Alikiba linaanza lilikuwa ni bifu kubwa sana Kutokana na ushindani ulio kuwepo,Clouds walijitahid kukuza bifu lile ili angalau kumpunguza nguvu Diamond,kweli kipindi cha mwanzoni lile bifu Nahisi Hata Mond Mwenyewe lilimtetemesha kidogo japo hakutaka kujionyesha wazi,
Hilo bifu liliendelelea ila mwisho wa siku mshindi alikuja kupatikana ambaye kila mmoja anamjua Ni Simba AKA Dangote,Moja ya sababu kubwa za Alikiba kushindwa ni Kutokana na mziki wake kutokuwa na ubunifu,pia utoaji wa nyimbo ukawa ni hafifu kwa madai kuwa nyimbo zake zina ishi so hawez kutoa track kila muda,Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa upande wa pila ambaye ni mshindani wake,Diamond Platnumz,yeye aliamini kabisa mziki ni biashara na kama ni biashara lazima ahakikishe walaji wake (Mashabiki) kila baada ya muda flani awape Chakula kipya,Mtindo huo wa Alikiba ilifikia hatua Hata wanao msapoti waachane naye wakiwemo clouds wenyewe wakabaki wanamsapoti kishingo upande,
Mpaka Muda huu Mziki huu wa bongo hauna ushindani tena Bali wamebaki wale wanao mchukia Diamond na kujifanya eti wao ni team mziki mzuri (Team kiba).
Kwa mtazamo wangu hapo juu ni kuwa Harmonize kwa uwezo alionao ni kwamba ana uwezo kwa 70℅ kumtetelesha Diamond endapo akichanga karata zake vizuri,Harmonize anacho takiwa kufanya ni kuwa karibu na clouds na kwa uwezo alio nao wa kuimba na kuachia song back to back naona kabisa Clouds wanamhitaji Konde boy kuliko Alikiba,Alikiba hakuwa chaguo sahihi Bali Jamaa alibebwa na wanao mchukia Diamond ila hawakuwa mashabiki.
Simaanishi Harmonize Anaweza kuwa Sawa na Diamond ila akicheza vizuri Anaweza fika mbali coz Jamaa tayari ana connections na wasanii wengi kwa sasa tofauti na Rich mavoko aliye ondoka akiwa hajajijenga vizuri.
Harmonize Najua kwa Muda huu mfupi atayumba ila akichanga karata zake vizuri Anaweza kuwa mkubwa zaid ya alivyo kuwa WCB,Anacho takiwa kukifanya ni kusimama mwenyewe na kutumia njia zile alizo jifunza kwenye chuo (Lebo yake WCB).
Harmonize Hizo views ulizo kuwa unapata kule You tube hazikuwa zako Bali zilikuwa za Diamond so zisikuteteleshe na kukukatisha tamaa baada ya kuona zimepungua,Huu ni Muda wa kutengeneza views zako ili uone ukubwa wako.
JF
Source
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...