Siri nyingi hufichuka wakati ambapo binadamu anafariki kwani licha ya kuwa ni kinyume na itikadi kumuanika aliyeaga dunia, mambo mengine hasa ya kifamilia huwa vigumu kuyaficha.
Hayo ndiyo yalifichuka baada ya dereva mmoja wa bodaboda aitwaye Hassan Mafabi (51) mkazi wa Nakatundu Kangulumira nchini Uganda kufariki dunia kwenye ajali ya barabarani pikipiki yake kugongana na gari siku ya Jumamosi wiki iliyopita.
Bodaboda huyo alikuwa na wake 6 na watoto 30 licha ya kazi yake yenye malipo ya wastani hali iliyosababisha watu wengi kushangaa ni vipi aliweza kutekeleza mahitaji ya wake hao wote.
Wengi wamepigwa na butwaa baada ya matangazo kuwafikia kuhusu mchango wa kusaidia familia ya marehemu kwani ameacha wajane sita na watoto 30.
Hassan Mafabi mwenye umri wa miaka 51 alikuwa akiishi na wake hao sita na watoto wake na kuchapa kazi kama kawaida huku wengi wasijue kuwa alikuwa na familia kiasi hicho.
Kulingana na Ugandanz.com, Mafibi aliishi katika kijiji kimoja nchini humo tangu kifo chake barabarani ambapo aligongwa na gari.
Askofu wa kanisa la Mukono nchini humo alidhibitisha kisa hicho na kuwataka marafiki kujitokeza kuisaidia familia ya Mafibi kwani yeye ndiye alitegemewa kuilisha.
Wengi hata hivyo walishangaa ni vipi mwendesha bodaboda huyo aliweza kuwalisha wake hao pamoja na watoto 30 ikizingatiwa mapato ya biashara ya bodaboda ni ya wastani tu.