Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa hatua ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge na kuzuiliwa kugombea Ubunge kwa miaka mitano inalenga kumzuia kutowania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2020.
Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Vincent Mashinji mbele ya waandishi wa habari ambapo amesema kuna ibara inamfunga Lissu kugombea ndani ya miaka mitano, na inambana hawezi kugombea Urais wa Tanzania kama hana sifa za kugombea Ubunge Tanzania.
"Muda wote ambao Spika anadai Lissu hajui alipo, Bunge limekuwa likimlipa mshahara, hili jambo si la kawaida, na watanzania wote wanajua Mama Samia Suluhu alikwenda kumsalimia Lissu Nairobi, na alienda kumpatia salamu za pole kutoka kwa Rais.", ameongeza Mashinji.
Utakumbuka kuwa mapema Ijumaa iliyopita, Spika wa Bunge, Job Ndugai alitangaza kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kile alichokidai kiongozi huyo kuwa na mahudhurio hafifu ndani ya Bunge na hajulikani halipo zaidi ya kuonekana kwenye nchi mbalimbali za Ulaya na Amerika.
Source