Siku chache baada ya picha zake kusambaa akionekana na wabunge tofauti kwenye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, huku kukiwa na madai kuwa ameenda kudanga, mrembo anayetikisa na umbo matata katika mitandao ya kijamii, Jacqueline Obeid 'Poshy Queen' amevunja ukimya juu ya safari yake hiyo.
Poshy amesema kuwa anawashangaa sana watu wote wanaomjadili na kumsemea maneno mabaya na kuuliza kuwa yeye kwenda bungeni ni makosa.
"Mbona watu wana matatizo sana, yaani mimi kwenda bungeni ni matatizo jamani au sistahili? Kule kila mtu anakaribishwa kama mgeni wakati mimi kuna jambo lilinipeleka kule na nimejifunza vingi", amesema Poshy.
Poshy ameongeza kuwa asingependa kabisa watu waendelee kumjadili kuhusu yeye kwenda bungeni kwa sababu kila mtu anaruhusiwa kwenda, lakini alivyokwenda yeye ilikuwa kwa sababu maalum ya kipindi cha Bunge la Bajeti ambapo amesomea mambo ya usimamizi wa fedha katika Chuo cha IFM jijini Dar es salaam.
"Kule nilikwenda na mimi kuwasilisha mawazo yangu katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, licha ya kuhudhuria hata nilivyokutana na baadhi ya wabunge niliwaambia mawazo yangu na wamesema watayafikisha huko", ameongeza Poshy.
Katika habari zilizoenea, Poshy alidaiwa kuwa alikwenda jijini humo kudanga baada ya kupata mualiko na mbunge mmoja ambaye ana uhusiano naye. Poshy ametokea kujizolea umaarufu mitandaoni kutokana na umbo lake matata la namba nane ambalo inasemekana kuwa amelipata ghafla au ni la kutengeneza.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...