Monday, June 24, 2019

GGM WAKUSANYA BIL 13 KUPITIA KILI CHALLENGE

Washiriki wa Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanayo kwa jina la Kili Challenge 2019 wakishuka wakiwa na Bendera ya Taifa huku wakiimba nyimbo mbalimbali za hamasa mara baada ya kuhitimisha safari ya siku saba ya kupanda mlima huo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira pamoja na Mkuu wa mkoa wa Geita ,Robert Gabriel wakiwa wamepokea Bendera ya Taifa kutoka kwa washiriki 64 wa changamoto ya kupanda Milima Kilimanjaro ambapowashiriki hao waliipandisha bendera hiyo kileleni.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya mapokezi ya washiriki 64 wa tukio la Kili Challenge 2019 akizungumza mara baada ya kuwapokea.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ulipo Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Robert Gabriel akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea washiriki 64 wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi.
Baadhi ya Washiriki.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti wamiliki wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Simon Shayo akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Baaadhi ya Washiriki wa Changamoto ya Kili Challenge 2019.
Kaimu mkurugenzi wa  Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini,(TACAIDS),Jumanne Isango akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitoa burudani kwa kuimba nyimbo wakati wa mapokezi ya Washiriki 64 wa Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanayo kama Kii Challenge 2019 .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghira akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Robert Gabriel ,Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Mhandisi Aisha Amour pamoja na Makamu w Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti,Simon Shayo wakielekea kutembelea mabanda ya maonesho yaliyokuwepo katika lango la mlima Kilimanjaro la Mweka .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjao ,Dkt Anna Mghwira akimkabidhi Mkuu wa mko wa Geita ,Robert Gabriel kumbukumbu ya kishika Funguo ( Key Holder) wakati akitembelea moja ya mabanda ya maonesho yaliyokuwa katika lango la Mweka wakati washiriki wa Changamoto ya Kupanda Mlima Kilimanjaro (Kili Challenge 2019 ) wakishuka kutoka kilele cha Uhuru.Nyuma ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ni Makamu wa Raisi wa Kampuni ya AngloGold Ashanti wamilki wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita.Simon Shayo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na  Washiriki 64 wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro pamoja na kuuzunguka kwa Baiskeli kwa lengo la kuchangisha fedha za Mapambano dhidi ya Ukimwi mara bada ya kuwasili katika lango la Mweka .
Mgeni rasmi katika hafla ya kuwapokea Washiriki 64 wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kuuzunguka kwa Baiskeli kwa lengo la kuchangisha fedha za Mapambano dhidi ya Ukimwi ,Mkuu wa Mkoawa Kilimanjaro akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wenzake na wadau .

Na Dixon Busagaga.

.Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira,amewataka wageni kutoka Nje ya nchi, kwa ajili ya shughuli za kijamii, Katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, kuepuka kuingilia shughuli za mlima huo.


Mbali na hilo, Mkuu huyo pia aliutaka Uongozi wa Wilaya zinazozunguka Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA, kumaliza migogoro inayohusu eneo la hifadhi hiyo,ikiwemo ya Nusu Mail,ambayo imekuwa ikihusisha wananchi wanaozunguka eneo hilo.


Mghwira ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye hafla ya kuwapokea wanaharakati 64,waliopanda Mlima kilimanjaro,kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi,Kampeni ambayo imeandaliwa na Mgodi wa madini ya Dhahabu Geita (GGM).


"Ipo migogoro ya Nusu maili,ambayo imekuwa ikizungumzwa kila wakati lakini haiishi,niombe viongozi wa Wilaya na Tanapa,waimalize.Niombe pia wageni kutoka nje ya nchi,ambao wanakuja kwetu,kwa shughuli hasa za kijamii,kujifunza kutoka kwetu,na wasituingilie sana kwenye eneo hili"amesema Mghwira


Aliongeza kuwa"Kila wakati tumekutana na mazingira ya wageni kujiingiza  kwenye masuala ya mlima na shughuli zinazofanyika hapa na kutuletea utata mgumu,sababu tunaposhughulika na 
Wageni kutoka nje ya nchi,mahusiano yake yanakuwa tofauti kidogo na namna ya kufanya maamuzi"


Mkuu huyo alitumia pia nafasi hiyo, kueleza kuwa,Ukimwi bado ni Tishio mtambuka na umegusa na kuathiri kila nyanja ya maendeleo na kuwataka wadau kushirikiana na serikali,kumaluza tatizo hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel,alisema katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa ukimwi,watoto wa Kike wameonekana kuwa wahanga wakubwa,na kuitaka jamii na wadau,kushiriki kulinda kundi hilo.


Kaimu mkurugenzi wa  Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini,(TACAIDS),Jumanne Isango, amesema kunahitajika ubunifu,ili kuongeza hamasa zaidi,katika kuupanda Mlima Kilimanjaro,kwa ajili ya kuchangisha Fedha za Mapambano dhidi ya Ukimwi.


Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti kupitia mgodi wa Dhahabu Wa Geita,Simon Shayo alisema zadi ya Bil 13 zimekusanywa katika kampeni hiyo tangu ianze na kuungwa mkono na zaidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali 40.

"Tunafurahi kweli na tunashukuru kwa washirika wetu wote na tutaendelea kushirikiana kufanya kila liwezekanalo na kwa ambao pia wangependa kujiunga katika vita hivi hii inamaanisha wakihamsika wapandaji zaidi itasababisha watu binafsi na jamii zaidi kuunga mkono na mpango wa Kili Challenge."alisema Shayo.

Shayo aliwashukuru wafadhili wa changamoto hiyo na wote walishiriki kupanda na kwamba jitihada walizoonesha ni muhimu katika kuchochea tukio hilo wakiwemo waendesha baiskeli ambao waliamua kuweka roho zao juu ili kuhakikisha Tanzania kupitia Kili Challenge inafikia sifuri 3 mwaka 2030.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...