Timu ya Mtibwa Sugar imetetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya kuwafunga wenyeji Azam FC kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.
Kipa Hatibu Waziri alitokea benchi dakika ya 119 kwenda kumalizia hatua ya matuta, akapangua mkwaju wa nne baada ya Azam kukosa tuta moja awali na Mtibwa wakatwaa tena taji hilo baada ya mwaka jana kufanya hivyo Dodoma.
Awali, Yanga SC ilifanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika michuano hiyo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Simba SC, mabao ya Kilaza Mazoea dakika ya 35 na Julius Wilson Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
Samwel Jackson wa Azam FC alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mashindano, Onesmo Mayaya Mfungaji Bora kwa mabao yake matano, Razack Ramadhan wa wote wa Mtibwa Sugar akawa Kipa Bora, Kocha Bora Said Maulid Kalikula 'SMG' wa Yanga SC na Refa Bora ni Ramadhan Kayoko wa Dar es Salaam.
Source
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
