Thursday, June 20, 2019
Hatuna nia ya kuwakomoa wananchi - Mkurugenzi wa BAWASA
Na John Walter-Babati .
Mkurungenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Babati (BAWASA) Idd Msuya amewataka wananchi kuacha kulalamika kuhusu kupanda kwa bei ya maji kwa unit kutokana na uhitaji mkubwa wa fedha za kuendelea kushughulikia miradi mingine ya maji kwenye sehemu ambazo zina uhaba wa maji.
Akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake mtaa wa Miomboni Mjini Babati, Mkurugenzi Mtendaji wa BAWASA Mhandisi Iddy Msuya alisema kuwa ongezeko hilo la asilimia 36 ni sawa na bei ya shilingi 1,748 kwa unit moja ya maji, bei ambayo ni ndogo ukilinganisha na mikoa mingine.
"Sisi kama BAWASA lengo letu la kupandisha bei ya maji hatuna nia ya kuwakomoa wananchi wetu hapana hii ni kuweza kupata fedha za kuweza kukarabati miundombinu ya maji ili ile kero ya kukatika kwa maji ifutike kabisa ili hata mtu akiamka usiku wa manane akifungulia maji yanatoka.
"Bei ya maji katika mkoa wa Arusha wenye chanzo cha maji ya mtiririko ni Shilingi 1,500 kwa unit moja sawa na asilima 50 ya ongezeko la bei ya maji hivyo Babati bado iko vizuri" Alisema Msuya.
Kwa mujibu wake hali ya upotevu wa maji imepungua na kufikia asilimia 35 kutokana na juhudi ya mamlaka ya BAWASA kuboresha miundo mbinu ya mabomba ya zamani ambayo baadhi yao iliwekwa katika kipindi cha Uhuru ambayo imechoka na kupoteza maji mengi.
Alisema kwa utaratibu BAWASA inapotaka kuongeza bei ya maji kwa walaji wake huomba mapendekezo ya ongezeko hilo la maji EWURA ambao huchukua mapendekezo kutoka kwa wadau na kuyapeleka Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa ajili ya kutoa kibali cha ongezeko hilo.
Mhandisi Msuya alifafanua kuwa BAWASA walipendekeza kuongeza bei kwa shilingi 2,175 kutokana na gharama za uendeshaji lakini baada ya kukusanya maoni ya Walaji na EWURA bei pendekezwa ilikuwa ni Shilingi 1,748 bei ambayo haikufanikiwa.
Msuya alibainisha kuwa kupanda kwa bei ya maji huwa inatolewa maelekezo mfano kununua mita za maji zipatazo 5,000, kuongeza mitandao ya maji kutoka Ng'wang'warai kuelekea shue ya msingi Tarangire na kujenga machujio ya maji ya kijiji hicho na Mutuka.
hata hivyo alisema ni azma ya serikali ya kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 upatikanaji wa maji ufikie asilimia 100 kwa wananchi waishio vijijini na kwamba BAWASA imejiwekea lengo la kuhakikisha wakazi wake wanapata maji kwa uhakika bila mgao au kulazimika kuchota maji.
Baadhi ya wananchi wa mji wa Babati walisema BAWASA haijawatendea haki kwani hawakushirikishwa kuongezeka kwa bei ya maji huku huduma ikiwa hairidhishi kwani hakuna mabadiliko ya huduma kwa kuwa maji yanayotoka ni machafu.
"Maji yanayotoka na ndio tunayoyatumia kwa kunywa, tunakunywa maji machafu sana wametupandishia bei ya maji lakini huduma ndo imezidi kuwa mbaya zaidi, maji yanatoka machafu na tulishawaambia wakasema watafuatilia lakini hadi leo kimya watatusababishia tuumwe matumbo," Alisema Yusufu Mdoe.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...