Sunday, June 23, 2019

APL YA KIGOMBE MABINGWA WA LIGI YA AWESO CUP PANGANI

Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe kushoto akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya APL ya Kigombe ambao ni Mabingwa wa Ligi ya wilaya ya Pangani Maarufu kama Aweso Cup kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso (CCM) Ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji .
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa ameshika kitita cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wa mashindano hayo kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Handeni
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza kwenye fainali ya Ligi ya Aweso Cup 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif akizungumza wakati wa fainali hizo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akiwa amebebwa na baadhi ya wapenzi na mashabiki wa soka wilayani Pangani mara baada ya kumalizika Ligi ya Aweso Cup
Katibu wa Kamati ya Mipango na fedha wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri kushoto akizungumza wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye jukwaa kuu na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson George wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Ligi hiyo
Kikosi cha timu ya Wa2020 wakiwa kwenye Picha ya Pamoja
Kikosi cha timu ya APL ya Kigombe 
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria fainali hiyo
Sehemu ya mashabiki wa soka wilayani Pangani wakifuatilia mashindano hayo
Wapenzi na mashabiki wa timu ya APL ya Kigombe wakishangia ushindi huo
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Ligi hiyo
TIMU ya APL FC ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga imetawazwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Wa 2020 FC mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa soka Kumba. 

Kutokana na Ubingwa huo APL Kigombe walifanikiwa kukabidhiwa Kombe la Mashindano hayo, Kitita cha Sh.Milioni moja na Ngom'be huku mshindi wa pili wa 2020 FC akipata kitita cha sh.laki sita na elfu sabini ya mbuzi na medali za dhahabu. 

Mshindi wa pili kwenye Mashindano hayo timu ya Wa 2020 FC walikabidhiwa medali, kitita cha laki sita, mbuzi na medali ya dhahabu kwa wachezaji wake huku mshindi wa tatu naye akipata kitita cha sh.laki nne na mbuzi. 

Mashindano hayo yamedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji huchezwa kila mwaka yakiwa na lengo la kuibua na kukuza viwango vya soka mkoani humo ambayo yalishirikisha timu 16. 

Mchezo huo wa fainali ya Ligi hiyo ulichezwa kwenye viwanja vya Kumba mjini Pangani uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wasanii wa bongo movie. 

Katika mchezo huo mabao ya APL ya Kigombe ambao ndio mabingwa wapya yalifungwa na Malimo Magembe kwenye dakika ya 35 baada ya kutumia uzembe wa mabeki wa timu pinzani kupachika wavuni bao hilo. 

Baada ya kuingia bao hiloWa 2020 FC waliweza kurudi kujipan ga na kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa APL ya Kigombe bila mafanikio kutokana na mashuti waliokuwa wakijipa wachezaji wao kugonga mwamba na kutoka nje. 

Shambulio hilo liliweza kuwaamsha APL Kigombe ambao baada waliweza kurudi kujipanga na kupelekea mashambulizi langoni 

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi Naibu Waziri Aweso alisema kwamba Ligi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani imewezesha kupandisha timu nne kwenye Ligi ya mkoa na baadae anaamini zitafika Ligi Daraja la kwanza na hatimaye Ligi kuu 

Alisema kupitia michezo wilaya ya Pangani inaweza kutoa wachezaji nguli kwenye soko kama vile Mbwana Samata na Thomas Ulimwengi ambao wanaweza kuitangaza nchi kupitia soka 

Aidha aliwataka kuendelea kushikamana na kupendana huku akikitaka Chama cha mpira wilayani Pangani kianzishe mashindanbo kwa upande wa wanawake ikiwemo rede na mpira wa miguu atadhamini. 

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Mipango na fedha wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri alisema kwamba kupitia mashindano ya Aweso Cup wameona vipaji vya wachezaji huku akieleza watachukua wachezaji 10 ambao watawatumia kwenye Ligi kuu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...