MAPOROMOKO ya udongo yaliyotokana na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 60 katika mikoa ya Durban na KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
Zaidi ya watu 1,000 wameondoka kutoka makazi yao kwa mujibu wa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ambaye ametembelea maeneo yaliyoathiriwa.
Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo siku chache zilizopita. Mafuriko zaidi na upepo mkali unatarajiwa katika maeneo ya pwani huku onyo likitolewa kuhusu hali mbaya ya hewa.
Mafuriko hayo makubwa yaliharibu biashara na nyumba za watu na vyuo vikuu viwili – huku mamia ya watu wakiondoka katika makazi yao.
Ramaphosa amezitembelea familia zilizopoteza wapendwa wao katika mafuriko hayo. Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko amesema kuwa rais aliweka shada la maua katika eneo ambalo watu wanane walifariki.
Pia alionekana akiwasukuma walinzi waliokuwa wakiwazuia watu kusema naye.
"Ni muhimu kuja kuona kile kilichofanyika au kilichotokea na kuomboleza na familia zilizopoteza wapendwa wao katika janga hili. Kupoteza maisha sio jambo rahisi, hasa maafa yakitokea ghafla," alisema Ramaphosa.
Wakati hayo yakijiri, Waziri wa Tawala za Mikoa, Nomusa Dube-Ncube, amewaambia maofisa wa kituo cha radio cha SAFM kwamba bado wanaendelea kutathmini kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mkasa huo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Siku zijazo watu watalazimika kuhamishwa kutoka maeneo yaliyoathirika, alisema. Watu kadhaa wamepelekwa hospitali huku shughuli ya kuwatafuta manusura waliyozikwa chini ya vifusi vya majengo yalioporomoka.
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...