Idara ya uhamiaji Mkoani Kagera imewakamata Tumaini Fransic na Peace Fransic raia wa nchi jirani ya Rwanda waliokuwa wanaishi hapa nchini kinyume cha sheria na kujifanya wWtanzania ambapo wameweza kupata elimu ya msingi, sekondari na chuo kikuu na kujipatia vyeti vya uraia kwa njia ya udanganyifu.
Mrakibu msaidizi wa Uhamiaji, Butenye Pendo amesema kuwa raia hao walizaliwa hapa nchini baada ya mzazi wao mmoja kuishi nchini kisheria ambaye ni mama yao mzazi lakini baada ya kumaliza elimu ya msingi na kujiunga na sekondari waliweza kutafta vyeti vya uraia ambapo mwenyekiti wa kijiji kyagati bw, Joseph Enerco Kanyonyi na wanawake walili Frida Samweli Kagemulo na Beatrice John Rweyemamu kujifanya wazazi wa watoto hao ili waweze kupata vitambulisho vya uraia na kuweza kupata mikopo ya elimu ya juu.
Afisa Pendo amesema kuwa Frida Samweli Kagemulo alisimama kama mama mzazi wa Tumaini Fransic na Beatrice John Rweyemamu kusimama kama mama mzazi wa Peace Fransic na mwenyekiti kuwasainia ili waweze kupata mikopo ya elimu ya juu kitendo ambacho kilifanikiwa huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
Amesema kuwa sheria ya uraia namba 357 iliyofanyiwa marekebisho yake mwaka 2002 inaelezea aina za uraia ulipo hapa nchini kuwa ni; Uraia wa kurithi, Uraia wa kuzaliwa na uraia wa kuandikishwa ambapo mtu anaomba uraia wa kuishi hapa nchini kwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria.
Bw, Pendo amesema kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani na kujibu tuhuma zinazowakabili huku akiwataka wananchi kuacha tabia za kuficha watu wasio wajua kwani wanaweza kujikuta wanakaribisha waharifu na majambazi ambao badae wanaweza kuvuruga amani waliyo nayo katika maeneo yao hasa watu wanaoishi mipakani.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 29, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...