Ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege ambao unasababishwa na vimelea aina ya paramyxovirus.
Kuenea kwa Ugonjwa
Ugonjwa wa Mdondo (Newcastle disease) huenea kupitia njia mbalimbali kama zifuatazo:-
- Mayai ya kuku aliyeugua ugonjwa wa mdondo/kideri (Newcastle disease).
- Kugusana na kuku mgonjwa.
- Kupitia maji yenye maambukizi.
- Wakati wa utotoleshaji vifaranga.
- Chakula chenye maambukizi.
- Hewa yenye maambukizi ya ugonjwa huu.
Dalili za Mdondo/Kideri (Newcastle disease)
- Vifo vya ghafla.
- Kutoa udenda mdomoni.
- Kukosa hamu ya kula.
- Kuharisha kinyesi cheupe na kijani.
- Kuhema kwa shida.
- Kukakamaa viungo au kupooza hasa mabawa, shingo na miguu.
- Kupunguza utagaji.
- Vifo hutegemea kasi ya ugonjwa huweza kufikia hadi asilimia mia moja (100%).
Namna ya kudhibiti Mdondo/Kideri (Newcastle disease)
- Wapewe chanjo kwa muda unaofaa (Siku ya 7 na 28, na kila baada ya miezi 3).
- Kuku wote waliozidiwa (wagonjwa) wachinjwe na wafukiwe katika shimo lenye kina kirefu kuzuia kuenea ugonjwa.
- Fuata maelekezo ya Daktari au Mtaalam wa mifugo.
Matibabu
Hakuna matibabu ya ugonjwa huu, ila kwa msaada na ushauri zaidi katika ufugaji wasiliana na Daktari au Mtaalam wa mifugo.
Source