Monday, March 25, 2019

Mbunge Gekul atamani Msanii mkubwa kutoka Babati


Na. John Walter, Babati

Mbunge Wa Jimbo la Babati  Mjini, Paulina Gekul ameahidi kuwapa ushirikiano wasanii wa Babati pindi watakapohitaji msaada kutoka kwake ili waweze kufikia malengo yao.

Ametoa ahadi hiyo wakati wa Tamasha maalumu la wasanii wa Babati ambalo lilienda sambamba na kukitambulisha kikundi cha wasanii wa kizazi kipya kijulikanacho kama GOOD MUSIC kinachosimamiwa na Msanii Dulla wa Dom ambapo pia alikabidhi shilingi laki tano kwa kikundi hicho.

Aidha amewashauri ili kuendelea kujulikana na kuwa na jina kubwa washirikiane na wasanii wenye majina ambao tayari wamepata mafanikio.

Tamasha hilo lilifanyika katika uwanja wa mpira Kwaraa kwa kujumuisha wasanii wa ndani na nje ya Babati.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mbunge Paulina  amewataka wasanii wa Babati kuwa na UPENDO,MSHIKAMANO na UMOJA ili kufikia mafanikio na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafika mafanikio ya juu katika sanaa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Babati Mjini, Mohammed Kibiki nae na ameahidi kushirikiana na wasanii hao  ili wapige hatua zaidi katika mafanikio ya kwenye sanaa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...