Friday, March 22, 2019

Alichosema Jerry Muro leo kuhusu Yanga SC na Haji Manara

Alichosema Jerry Muro leo kuhusu Yanga SC na Haji Manara
Aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC, Jerry Muro amezidi kuonyesha kuwa bado anahitaji kutumika kwenye soka.

Amebainisha hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Kipenga Xtra cha East Africa Radio ambapo ameeleza kuwa bado anahitaji kupambana na msemaji wa Simba SC, Haji Manara.

"Tofauti yangu mimi na Manara ni kwamba mimi  ni mtabiri, mtu wa Mungu. Nikisema linakuwa,
sio Manara anakwenda kwenda tuu  na ninasema kama juzi ilikuwa 'Do 0r die' basi sasa itakuwa
kufa na kuzikana," amesema Jerry.

Ameendelea kwa kusema kuwa, 'Hakuna kitu nakipenda kama kufanya kazi Yanga, natamani
ningeruhusiwa na Rais Magufuli nifanye kazi Yanga kwa 'party time'. Nikimsikia Manara
anaongea huwa natamani nipae nije nimdhibiti huyu Manara, mwenyewe anajua mafahari wawili
hawakai zizi moja'.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...