Monday, February 18, 2019
Yondani Afunguka Kutompa Mkono Ajibu
BEKI mkongwe wa kati wa Yanga, Kelvin Yondan i amefuta ukimya na kufungukia ishu yake ya kutopeana mkono na nahodha wake, Ibrahim Ajibu.
Hiyo, ikiwa ni siku moja tangu iibuke taarifa za wachezaji hao kutokuwepo katika mahusiano mazuri baada ya video kusambaa ya Yondani kukataa kumpa mkono Ajibu.
Kitendo hicho kilitafsiriwa na wengi kuwa Yondani ana kinyongo na Ajibu, baada ya kuvuliwa unahodha na mikoba yake kukabidhiwa kiungo huyo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati Ajibu akiwatambulisha wachezaji wake kwa mgeni rasmi wakati Yanga ilipocheza mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba juzi, Dar.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Yondani alisema hakuna bifu lolote kati yake na Ajibu huku akitaja uchochezi wa mashabiki ndiyo umesababisha minong'ono kuhusu tukio hilo.
Yondani amedai kuwa hakumpa mkono Ajibu kama masihara tu, kwa kuwa siyo utaratibu wa nahodha kushikana mikono na wachezaji wakati akiwatambulisha.
"Mimi Ajibu ni mdogo wangu na mara nyingi tumekuwa tukitaniana ndani na nje ya uwanja na hilo tukio la mimi kukataa mkono wa Ajibu nilijua ni masihara ananiletea, ndiyo maana nikakataa kumpa mkono.
"Kwa sababu Ajibu katika mechi zote za ligi ambazo tumezicheza hajawahi kutupa mikono wachezaji, yeye anaishia kututambulisha majina yetu na mgeni rasmi ndiyo anatupa mikono, hivyo nashangaa suala hilo linavyochukuliwa.
"Kama ningekuwa na bifu au chuki na Ajibu, basi nisingekuwa nampa ushauri na siyo huyo, wachezaji wengi wanafuata ushauri kwangu kutokana na ukongwe nilionao wakiwemo baadhi Samatta (Mbwana), Msuva (Simon) na Banda (Abdi), hivyo niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga katika hilo, mimi sina ugomvi na Ajibu," alisema Yondani.
Championi Jumatatu, lilimtafuta Ajibu kuzungumzia hilo simu yake iliita bila kupokelewa lakini taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo haijathibitishwa kama ni ya Ajibu, inamnukuu hivi:
"Nahisi wenzangu walinishangaa kuwatambulisha kwa kuwashika mkono, mara nyingi huwa hatufanyagi hivyo, Yondani ni kaka yangu na siyo yeye pekee pia Dante (Andrew Vicent), Yondani alisita na kuniambia hii mpya. Sina shida na kaka yangu huyu, sisi ni wadogo zake na mengi tunajifunza kwake."
WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
