Monday, February 18, 2019
Naibu Waziri, Kanyasu ataka ujenzi Ihumwa utumie zaidi vyuma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametaka ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali yanayojengwa katika eneo la Ihumwa yajikite kutumia vyuma badala ya kutumia mbao ngumu ambapo kwa sasa Wizara ipo kwenye kampeni kubwa ya kuzuia matumizi ya miti hiyo ambayo ipo hatarini kutoweka
Amesema Wizara kwa sasa imepiga marufuku ukataji na usafirishaji wa magogo yanayozalisha mbao ngumu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri huyo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua hatua za ujenzi wa jengo hilo unaoendelea jijini Dodoma.
Aidha, Kanyasu ameshauri Jengo la Wizara hiyo lisitumie nguzo za mbao kwa upande wa mbele katika sehemu ya kuingilia kama inavyoonekana kwenye ramani badala yake itumie nguzo za zege ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Pia, Constantine Kanyasu ametaka timu ya wataalam mbalimbali ifanye kazi kwa pamoja katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa jengo hilo la Wizara katika mji wa Kiserikali wa Ihumwa.
Amesema licha ya kuwa hatua ya ujenzi wa jengo hilo ni ya kuridhisha ila ametaka nguvu ziongezwe ili kuweza kulikamilisha jengo hilo ndani ya muda wa wiki mbili zijazo licha ya kuwa muda uliotolewa na Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa tayari umeshapita.
Katika nyingine, Kanyasu ameshauri hatua za kupanda miti pamoja kuandaa bustani za maua zianze mapema katika jengo hilo ili likishakamilika liwe kwenye madhari nzuri badala ya kusubili hadi pale jengo litakapokamilika kabisa.
Kwa upande wake, Mkandarasi wa Suma JKT, Clement Shaibu amemueleza Naibu huyo kuwa ujenzi unaendelea vizuri na wanatarajia kukamilisha ndani ya wiki mbili zijazo.
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 29, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...