Ukiachana na tetesi na kesi anayokumbana nayo ya kuambiwa kuwa anatumia madawa ya kulevya aina ya bangi lakini pia msanii huyo pia amekumbwa na tetesi ya kutaka kutoka katika lebo ya wcb na kusemekana kuwa anataka kufungua lebo yake. Harmonize ambae anaweza kuwa ndio msanii mkubwa ndani ya WCB akitoka Diamond , amekanusha taarifa hizo za kutaka kutoka katika lebo hiyo huku akikataa kutoa taarif zaidi ya swala hilo. Mwanamuziki huyo ambae kwa sasa amekumbwa na tetesi hizo za kuvuta bangi , huku kesi hiyo ikiwa imekwishafika kwa Mkuu wa mkoa , alitafutwa na gazeti la Amani lakini alikataa kusema swala hilo na kukata simu yake. Hata hivyo baada ya kuwakatia simu waandishi wa habari waliamua kumtafuta meneja wa wasanii owte ili kutaka kujua kama ni kweli Harmonize anatarajia kuondoka katika lebo hiyo karibuni, lakini alipokea na alipokutana na swali aliahidi kupiga baadae lakini hakufanya hivyo tena. hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyo kusikika akitaka kuhama katika lebo hiyo.
The post Ni kweli Harmonize Ataka Kutoka WCB appeared first on Ghafla! Tanzania.
Source