Saturday, February 16, 2019
Kama unataka kudumu katika mahusiano yako epuka kumwambia mpenzi wako maneno haya
Endapo umekwisha ingia katika mahusiano au unatarajia kuingia katika mahusiano ya kimapenzi, yapo mambo yanyofaa ambayo junaweza kumwambia mpenzi wako naye akafurahi, lakini yapo mambo ambayo kimsingi hupaswi kabisa kumwambia mpenzi wako. Kwani endapo utaamua kumwambia utatengeneza njia ambayo itawafanya mahusiono yenu yafe mara moja.
Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vyema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile.
Maneno Mabaya Ambayo Hutakiwi Kusema Kwa Mwenza Wako:
1. Nakuchukia
Chuki ni kitu kikubwa sana,kwa kweli huwezi kuishi na mtu ambaye unamchukia. Hutakiwi kumtamkia mwenza wako neno hili. Unaweza kuchukia tabia yake lakini si yeye mwenyewe. Njia nzuri ni kusema kuwa "Nachukia au sipendi tabia yako ya kuchelewa kurudi nyumbani" au maneno yanayofanana na hayo.
2. Maneno ya Matusi
Maneno kama "mjinga" au "mpumbavu" yasitumike kwa mwenza wako hata kama yana ukweli ndani yake. Japo ujinga ni kutofahamu kitu fulani lakini neno hili linaleta majeraha kama likitoka kwa mwenza. Hasa kama linatoka wakati wa ugomvi au kutofautiana.
Useseme maneno mabaya yanayomshusha mweza wako mfano kuhusu mwonekano mbaya wa mwenza wako kama "sura mbaya","Mnene kama nguruwe" n.k
3. Kumfananisha Tabia Mbaya mwezi wako na Wazazi Wake.
"Tabia zako kama mama yako", au "..kama baba yako" maneno yanayomfananisha mwenza wako na wazazi au familia anakotoka yanachokoza sana na huweka vidonga kwa muda mrefu moyoni na yaepukwe.
4. Acha! Nitafanya Mwenyewe
Katika mahusiano kusaidiana ni jambo la kawaida na muhimu,maneno mabaya ya namna hii yanamvunja moyo mweza wako kutaka kufanya jambo kwako siku nyingine na linaleta utengano na kuvunjika kwa upendo.
5. Maneno Mabaya ya Kukatisha Tamaa
"Hutaweza" ,"Hutafanikiwa" n.k yanavunja moyo kwa mwenza wako na kurudisha nyuma maendeleo.
Ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote muende mbele kwa pamoja. Umoja ni nguvu.
Hivyo nikusihi ya kwamba kama kweli unataka kudumu katika mahusiano ya ndoa acha mara moja kumwambia maneno hayo, bali unatakiwa kumfariji kwa maneno mazuri yenye kuleta upendo wa kweli na kujenga hamasa ya kudumu milele.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
