Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tabora imewapandisha kizimbani Watumishi 7 wa halmashauri 3 za mkoa wa Tabora kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa taaasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Tabora, Mogasa Mogasa amesema kuwa katika kipindi cha Julai-Septemba 30 mwaka huu, jumla ya malalamiko 28 ya rushwa yalipokelewa na Taasisi hiyo na kufunguliwa mashtaka na sita kati yake yamefikishwa mahakamani.
Mogasa amewataja watuhumiwa wa shauri hilo la uhujumu uchumi kuwa ni Bikilile Mahyenga (Kaimu Mweka hazina) na Andrew Ndaba (Mhasibu) wanaokabiliwa na mashitaka mawili ya kughushi na kupokea rushwa.
Amesema kesi nyingine ni cc na.74/2018 dhidi ya Stephen Nyanda aliyekuwa Mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Uyui ambaye shauri lake lipo kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Tabora Sarafina Nsana na linatarajiwa kutajwa Novemba 28 mwaka huu.
Mogasa amemtaja mtuhumiwa mwingine aliyefikishwa mahakamani kuwa ni Emanuel Mwakasumule aliyekuwa Katibu wa Baraza la Ardhi kata ya Ziba wilaya ya Igunga ambaye anakabiliwa na kesi ya rushwa na. 1/2018.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...