Friday, November 2, 2018
Mke Wangu Kanichezea Umafia Huu Baada ya Kutaka Kuchepuka...Kanifuata Mpaka Morogoro
Enzi hizo niko na wife. Nishamuaga tangia siku tatu nyuma kua Jumapili nitasafari kikazi kwenda Morogoro kwa muda wa siku tatu. Huku mimi nilikua nishapanga na sweetie wangu Mboni kwamba tunaenda kula bata Morogoro kuanzia hiyo Jumapili hadi jumatano yake! Tukakubalianaa nimpitie kituo cha bus Kimara Baruti
Wife alikua kanifungashia vizuri sana nguo zangu na mahitaji mengine ya safari katika bag langu(wanaume tunadhambi saa zingine!). Na ilipofika muda wa safari akanitaka nimpe lift nimuache salon akatengeneze nywele zake
Tulipofika hapo salon akataka nimsubiri dakika tano tu aangalie kama kuna foleni maana alikua hajawapigia simu, na baada ya muda huo akaja akanambia bado kuna foleni kwahiyo nimpe lift hadi stand ya mkoa kuna parcel katumiwa toka Tanga na mama yake na kashapigiwa simu akaifuate
Nilipofika maeneo ya stand ya mkoa akanambia "Twende hadi TANESCO Ubungo nitashuka nifanye mazoezi ya kutembea, nitarudi kwa miguu hadi stand ya mkoa". Ile nataka ku park ashuke hapo TANESCO akanikataza akasema "Twende tu nitakwambia nitaposhukia"
Ikabidi ninyooshe tu huku nina wasiwasi kibao nikijiuliza bila majibu nini kinachoendelea! Tulipofika Baruti nikapiga jicho pale kituoni huku kiroho kinanidunda, nikamuona Mboni amekaa pale stand na akawa ameiona gari ila wife hakuonekana kama ameshtukia kitu chochote. Nikaichukua simu yangu nikajifanya kama napiga nikaitoa mlio maana nikahisi Mboni angepiga
Tulipofika Mbezi mwisho nikamwambia wife huoni kua unakuja mbali sana? Akanijibu "Nimekwambia Sesten wee twende nitakapotaka kushuka nitakwambia" Sikumuuliza tena wapi atashuka na huwezi amini tulifika hadi Moro tukaingia Morogoro Hotel kama saa kumi na mbili kasoro hivi
Bahati nzuri kulikua na mabango yanayoonyesha kuna taasisi kadhaa zina semina, workshops na training hapo hotelini na mimi nikambabatiza muhudumu kwa kumwambia kumbe taasisi hii wanafanyia ukumbi wa Chief Kingalu? Wife akasikia nilivyojibiwa "Ndiyo" maana na yeye alishuka kwenye gari na kunifuata counter, kisha tulichukua room
Nikawa kazi yangu tukiamka asubuhi mimi natoka nasema naenda ukumbini kumbe napitiliza hadi town naenda sehemu nyingine kabisaa, tena bila gari huku yeye anabaki hotelini na wakati mwingine anatoka na gari anaenda tu kuzurura mjini. Bahati nzuri nilipo mpigia Mboni na kumweleza yaliyonipata alinielewa akasema "Nilimuona dada kwenye gari ndio maana hata sikupiga simu"
Ilipofika J5 tuka check out na kurudi zetu Dar na wala hakukua na dalili yoyote ya ugomvi, kununiwa au wasiwasi, kitu ambacho kinafanya nijiulize hadi leo kua hivi yule mwanamke alikua anafikiria nini? Alitaka kunifanyia surprise? Alihisi anaibiwa? Au alitakatu kubadilisha location na scene ya kugegedana? Maana sio kwa umafia ule aisee!
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...