Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu imemchagua Kocha wa Azam FC, Han Pluijm kuwa Kocha Bora wa mwezi Oktoba akiwashinda Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nsazwarimo.
Pluijm aliiongoza timu yake kupata pointi 15 baada ya kushinda michezo yote mitano iliyocheza na kushika nafasi ya kwanza, huku Aussems akiiongoza Simba kushinda michezo yote minne iliyocheza hivyo kupata pointi 12 na kushika nafasi ya pili, wakati Nsazwarimo alipata pointi 11 akishinda michezo mitatu na kutoka sare mitatu akiiwezesha timu yake kupanda hadi nafasi ya nane.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo, ambapo msimu wa mwaka 2017/2018 kulikuwa tuzo 16 zilitolewa kwa washindi wa kada mbalimbali, ambapo kwa ushindi huo Okwi atazawadiwa tuzo, king'amuzi kutoka Azam na Sh milioni moja kwa kuibuka Mchezaji Bora wa mwezi.
Washindi wengine wa tuzo hiyo kwa msimu huu na miezi yao katika mabano ni mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na mshambuliaji wa Mbeya City Eliud Ambokile.
Kwa upande wa makocha walioshinda tuzo hizo kwa msimu huu ni Amri Said wa Mbao FC aliyeshinda tuzo ya Kocha Bora wa Agosti na Mwinyi Zahera wa Yanga aliyeshinda tuzo ya Kocha Bora wa Septemba.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akitoa hotuba yake kwa wageni mbalimbali waliohudhulia dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumk...
-
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kuanzia kesho Jumatano Juni 23, 2021 itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia eneo la hospita...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mjasiriamali Faiza Ally ameweka wazi hisia zake na kusema kuwa anatamani sana kuona msanii wa Bongo Flev...
-
UNAPOTAJA jina la mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' kutoka Tanzania, akili za wengi zinakimbilia kwe...
-
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya siku tano ya kunyesha mvua kubwa inayoweza kusababisha athari ikiwemo mafuriko. ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Geneva, Switzerland /AFP /.More than 100 groups urged the International Labour Organization to stop taking money from tobacco companies as t...