Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama mnavyofahamu linashiriki Ulinzi wa Amani ndani na nje ya Bara la Afrika.
JWTZ linasikitika kuwataarifu kwamba limewapoteza wapiganaji wake watatu (3) waliofariki kwa tarehe tofauti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika ya Kati (CAR) wakiwa kwenye jukumu la Ulinzi wa Amani baada ya kushambuliwa na vikundi vinavyosadikiwa kuwa ni vya waasi.
Mashujaa wetu waliouwawa ni Koplo Mohamed Mussa, Koplo Erick Masauri John na Praiveti Musa Shija Machibya. Miili ya marehemu hao tayari imepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuhifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.
Heshima za mwisho kwa mashujaa wetu hao zitatolewa katika sehemu ya kuagia Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kesho tarehe 23 Novemba 2018 kuanzia saa 2.30 asubuhi. Vyombo vya Habari na Wananchi wanakaribishwa tuungane katika kuaga mashujaa wetu.
Mungu azilaze Roho za Mashujaa wetu mahali pema Peponi, Amina
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
