Tuesday, November 27, 2018
Jinsi ya kuzuia mtoto mwenye tatizo la kukojoa kitandani
Mtoto kukojoa kitandani inazuilika na mara nyingine sio hata ugonjwa ni malezi tu. Ingawa mara nyingi huwa ni ugonjwa na huitaji ushauri wa daktari na hutibika kabisa.
Hapa tutaangalia njia za kuzuia mtoto kukojoa kitandani kwa wale ambao hawana matatizo ya kitabibu;
-Njia ya kwanza ni kuthibiti unywaji wa vimiminika masaa machache kabla ya kulala au wakati wa usiku. Hakikisha anaenda kukojoa kabla hajaenda kulala na ulisimamie hili.
-Njia ya pili ni kumuamsha wakati wa siku kwa ajili ya haja ndogo ili kuzuia kukojoa kitandani, mara kwa mara. Weka hata kengele ya kwenye saa ikukumbushe kila baada ya masaa mawili au matatu. Kesho yake akikojoa tena rudisha yale masaa na umwamshe baada ya lisaa limoja na nusu kila siku.
-Njia nyingine ni Asali mbichi, mpe mtoto kijiko kidogo cha asali mbichi kabla ya kulala kila siku, mpaka atakapo pona. Unaweza kumpakia kwenye mkate wakati wa chai asubuhi.
-Mdalasini pia ni dawa nzuri sana kwa watoto wenye matatizo ya kukojoa kitandani, huufanya mwili wa mtoto kupata joto ambalo huzuia kukojoa kitandani. Chukua unga wa mdalasini kijiko kidogo kisha changanya na asali halafu paka kwenye mkate au uchanganye kwenye maziwa fresh.
-Masaji, hii pia ni dawa nzuri kwa kuzuia kukojoa kitandani, tumia mafuta ya zeituni (olive oil) yachemshe kidogo yapate uvuvugu alafu mfanyie massage mtoto chini ya tumbo. Fanya ivo mara kadha, taratibu taratibu.
-Usimpige mtoto kwa sababu ya kukojoa kitandani wala kumfokea bali mlee kwa upendo na uwe unampa zawadi kila mara asipokojoa kumpa moyo. Pia usiku uhakikishe njia ya kwenda chooni ina mwanga wa kutosha kwa kua watoto huogopa giza pamoja na hilo msindikize mpaka atakapokua na uwezo wa kwenda mwenyewe. Fanya mambo kwa upendo nae atakua anaelewa na kuacha kukojoa kitandani. Kama hizo njia zote zikishindikana mpeleke kwenye kituo cha afya kwa matibabu zaidi.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
