Wednesday, October 24, 2018

Fahamu Faida za Manjano Katika Urembo

Manjano ni moja ya kiungo kinachotumika  katika mchuzi lakini pia imekuwa ikitumiwa a warembo kuweka ngozi katika hali ya usafi zaidi.Kwa wanaotaka kutumia ama urembo uwa na faida zifuatazo :- Hutibu chunusi– Manjano ina 'antiseptic' na 'anti-bacterial' ambazo husaidia kupambana dhidi ya chunusi na vidonda usoni na kukupa muonekano mzuri. Manjano pia husaidia kupunguza mafuta usoni kwa wale wenye nyuso zenye mafuta. Vinavyohitajika Liwa kijiko kimoja cha chai Manjano kijiko kimoja Juisi ya limau Changanya viungo hivi pamoja na kisha uipake usoni na ukae navyo kwa muda usio pungua dakika 10. Ili kuondoa chunusi, changanya manjano na maji safi kisha upake usoni na ukae hivyo kwa dakika 15 kabla ya kunawa uso wako kwa maji ya fufutende. mask kwa wenye nyuso zenye mafuta mengi– Manjanoina manufaa katika ngozi zenye mafuta na husaidia kupunguza mafuta na hio upelekea kupunguza chunusi usoni. Vinavyohitajika juisi ya machungwa liwa manjano Vichangaye vyote hivi kisha vipake usoni na ukae navyo kwa dakika kati ya 10-15 kabla ya kuosha. Mask kwa ngozi kavu– Kama una ngozi kavu, unaweza kutengeneza 'mask' kwa kuchanganya ute wa yai moja, mafuta ya mizeituni vijiko viwili vya chai, namanjano vijiko viwili. Mchanganyiko huu unaweza kutumia kwenye ngozi kavu kama vile usoni, shingoni, magotini. Ukishajipaka ni muhimu uache kwa dakika 15 au 20 kabla ya kunawa. Huondoa makunyanzi– Manjanoikichangaywa pamoja na viugo vingine ina ufanisi katika kuondoa makunyanzi usoni. Unaweza kuandaa mchanganyiko kwa kuchanganya unga wa manjano pamoja na mchele uliosagwa, maziwa na juisi ya nyanya na kupaka usoni na shingoni.Muda wa nusu saa ukishapita, unashauriwa kutumia maji moto kujiosha. Ukifanya hivi angalau mara moja kwa wiki uso wako utaanza kung'aa. Kuondoa michirizi (stretchmarks)Manjanohusaidia kufuta michirizi. Changanya manjano na maziwa au maji kisha upake katika sehemu yenye michirizi. Baada ya dakika 30, oga kwa maji ya fufutende kisha upake losheni.   Faida ya manjanokwenye nywele –Manjano husaidia katika ukuaji wa nywele, pia kuondoa mba. Changanya manjano na olive oil kisha...

Continue Reading

The post Fahamu Faida za Manjano Katika Urembo appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...