Namna ya kujaza nywele kwa njia za asili
Kunamtu amenitumia swali juu ya nini afanye ili Nywele zake ndefu ambazo ni chache, zijae.
Nataka kumwambia kwamba hilo linawezekana kwa kufanya yafuatayo.
- Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na kiini cha yai.
- Osha nywele zako kwa shampoo na uzikaushe.
- Ponda ponda parachichi mpaka lilainike kabisa. Chukua vijiko vitatu vya asali na kiini cha yai kisha changanya yote kwa pamoja.
- Paka mchanganyiko huo kaa nao kwa muda wa dakika 15 kisha osha.
- Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele yako.