Sunday, August 5, 2018
Wanachama wa Upinzani wakamatwa na kupandishwa mahakamani
Wanachama kadhaa wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe (MDC) wamefikishwa mahakamani jana Jumamosi wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya vurugu baada ya uchaguzi wa Jumatatu.
Wanachama hao wanaodaiwa kufanya vurugu katika ofisi za chama tawala pamoja na kuchoma moto magari wamerejeshwa mahabusu hadi ombi lao la kupata dhamana litakaposikilizwa kesho Jumatatu. Kiasi watu sita walifariki dunia baada ya wanajeshi kuwafyatulia risasi waandamanaji hatua iliyokumbusha kumbukumbu ya vurugu baada ya uchaguzi wakati wa utawala wa Robert Mugabe.
Mnangagwa amekishutumu chama cha Movement for Democratic Change- MDC kwa kusababisha vurugu na kuahidi kuunda tume huru kuchunguza mauaji hayo. Tume ya uchaguzi ilimtangaza Mnangagwa kushinda uchaguzi kwa asilimia 50.8 ya kura dhidi ya mgombea wa MDC Nelson Chamisa aliyepata asilimia 44.3 ya kura.
Mnangagwa mshirika wazamani wa rais Robert Mugabe ametoa mwito wa mshikamano ikiwa ni baada ya mshindani wake katika kuwania urais Nelson Chamisa wa chama cha MDC kuyakataa matokeo akisisitiza alikuwa ndiye mshindi katika uchaguzi.
Wakili wa upande wa utetezi Denford Helimani amesema wanaume 16 pamoja na wanawake wanane wamekamatwa ikiwa ni hatua dhidi ya upinzani.
Mnangagwa amekuwa akisisitiza kuwa uchaguzi wa Jumatatu ulikuwa huru na haki na kuusifia uchaguzi kuwa ni mwanzo mpya mnamo wakati akichukua hatua kukomesha kutengwa kwa Zimbabwe na Jumuiya ya kimataifa.
Waangalizi wa kimataifa wameusifu uchaguzi huo kuwa umefanyika kwa amani ingawa waangalizi wa Umoja wa Ulaya wanasema Mnagagwa alitumia taasisi za serikali pamoja na vyombo vya habari kushinda uchaguzi kutokana na kampeni za uchaguzi huo kutofanyika katika mazingira sawa ya huru na haki.
Chamisa mchungaji na mwanasheria mwenye umri wa miaka 40 ametoa mwito kwa wafuasi wake kujiepusha na vurugu wakati akitarajia kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.
Mnangagwa aliye na umri wa miaka 75 anasema Chamisa yuko huru kupinga matokeo hayo ya uchaguzi mahakamani ingawa hatua hiyo inaonekana kupewa nafasi kidogo kubadilisha matokeo.
Mshirika huyo wazamani wa Robert Mugabe alichaguliwa kuongoza chama cha ZANU-PF baada ya Mugabe kujizulu Novemba mwaka jana kufuatia shinikizo la jeshi baada ya kukaa madarakani miaka 37.
Makundi ya haki za binadamu yameonesha wasiwasi kuwa hatua ya polisi kutumia nguvu zaidi dhidi ya waandamanaji ni dalili ya jinsi anavyotarajia kutawala nchini humo.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
