Je unaujua mfuko mdogo katika suruali yako ya Jeans? Ndiyo, ule ambao umeshonwa juu kidogo ya mfuko mkubwa wa kulia.
Umewahi hata mara moja kusimama na kujitafakari kwa nini huo mfuko mdogo mbele ya suruali yako ya jeans upo hapo ulipo na nini hasa lengo la mfuko huo zaidi ya pengine kudumbukiza sarafu au jojo ambayo unataka kuja kuitafuna baadae au kuwaza kama ni fasheni tu katika nguo?
Kama hujawahi kujiuliza hilo swali na bado hujui chanzo na lengo la mfuko huo mdogo mbele ya suruali yako ya Jeans usijali kwani tovuti hii itakueleza chanzo na lengo la mfuko huo.
Mfuko huu ulikuwa unatekeleza jukumu muhimu sana miaka ya nyuma na ndio sababu kubwa iliyopelekea watengenezaji wa suruali za Jeans kuweka mfuko huo juu kidogo ya mfuko wa mbele wa suruali.
"Ni mfuko maalum wa kuhifadhi saa. Ndiyo, inasemekana miaka ya nyuma ya 1,800, watu wengi walikuwa wanapenda kuvaa saa zao katika cheni na kuzifungia katika viuno vyao. Ili kuweza kuweka salama saa zao zisivunjike na kuharibika, Levi, watengenezaji wa kwanza kutengeneza suruali za Jeans wakaamua kuweka mfuko huo mdogo mahali ambapo watu hao wangeweza kuhifadhi saa zao salama na kwa wepesi zaidi.
Hivyo ulianza kama mfuko wa kuhifadhi salama saa za mifukoni, japo baadae ukaanza kupata matumizi mengine kama kuhifadhia sarafu, tiketi za safari, kondomu, na viberiti hasa kwa watumia sigara.
Tangu hapo suruali za Jeans za aina zote zimekuwa zikitengezwa na mfuko huo mdogo bila kujali fasheni iliyopo kwa wakati huo.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
